Kwa ajili ya kuonewa kwao wanyonge, Kwa ajili ya kuugua kwao wahitaji, Sasa nitasimama, asema BWANA, Nitamweka salama yeye wanayemfyonya.
Isaya 29:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Wanyenyekevu nao wataongeza furaha yao katika BWANA, na maskini katika wanadamu watafurahi katika Mtakatifu wa Israeli. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wanyofu watapata furaha mpya kwa Mwenyezi-Mungu, na maskini wa watu watashangilia kwa furaha kwa sababu ya Mungu, Mtakatifu wa Israeli. Biblia Habari Njema - BHND Wanyofu watapata furaha mpya kwa Mwenyezi-Mungu, na maskini wa watu watashangilia kwa furaha kwa sababu ya Mungu, Mtakatifu wa Israeli. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wanyofu watapata furaha mpya kwa Mwenyezi-Mungu, na maskini wa watu watashangilia kwa furaha kwa sababu ya Mungu, Mtakatifu wa Israeli. Neno: Bibilia Takatifu Mara nyingine tena wanyenyekevu watafurahi katika Mwenyezi Mungu, wahitaji watafurahi ndani yake Aliye Mtakatifu wa Israeli. Neno: Maandiko Matakatifu Mara nyingine tena wanyenyekevu watafurahi katika bwana, wahitaji watafurahi katika yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli. BIBLIA KISWAHILI Wanyenyekevu nao wataongeza furaha yao katika BWANA, na maskini katika wanadamu watafurahi katika Mtakatifu wa Israeli. |
Kwa ajili ya kuonewa kwao wanyonge, Kwa ajili ya kuugua kwao wahitaji, Sasa nitasimama, asema BWANA, Nitamweka salama yeye wanayemfyonya.
Miisho yote ya dunia itakumbuka, Na watu watamrejea BWANA; Jamaa zote za mataifa watamsujudia.
bali kwa haki atawahukumu maskini, naye atawaonya wanyenyekevu wa dunia kwa adili; naye ataipiga dunia kwa fimbo ya kinywa chake, na kwa pumzi ya midomo yake atawaua wabaya.
Nao walio maskini kabisa watakula, Na wahitaji watajilaza salama; Nami nitatia shina lako kwa njaa, Na mabaki yako watauawa.
Wajumbe wa taifa hilo waletewe jibu gani? Ya kuwa BWANA ameiweka misingi ya Sayuni, na ndani yake wale walioonewa katika watu wake watapata kimbilio kwake.
Maana umekuwa ngome ya maskini, Ngome ya mhitaji katika dhiki yake, Mahali pa kukimbilia wakati wa tufani, Na kivuli wakati wa joto; Wakati kishindo cha watu wakatili kilipokuwa, Kama dhoruba ipigayo ukuta.
BWANA ataingia katika kuwahukumu wazee wa watu wake na wakuu wao; Ninyi ndinyi mliokula shamba la mizabibu; vitu mlivyowateka maskini vi ndani ya nyumba zenu.
Ni nini maana yake, ninyi kuwaonea watu wangu, na kuponda nyuso za maskini? Asema Bwana, BWANA wa majeshi.
Maana yeye aliye juu, aliyetukuka, akaaye milele; ambaye jina lake ni Mtakatifu; asema hivi; Nakaa mimi mahali palipoinuka, palipo patakatifu; tena pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu na kunyenyekea, ili kuzifufua roho za wanyenyekevu, na kuifufua mioyo yao waliotubu.
Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu BWANA amenitia mafuta niwahubirie wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwatibu waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao.
Nitafurahi sana katika BWANA, nafsi yangu itashangilia katika Mungu wangu; maana amenivika mavazi ya wokovu, amenifunika vazi la haki, kama bwana arusi ajipambavyo kwa kilemba cha maua, na kama bibi arusi ajipambavyo kwa vyombo vya dhahabu.
Maana mkono wangu ndio uliofanya hivi vyote, vitu hivi vyote vikapata kutokea, asema BWANA; lakini mtu huyu ndiye nitakayemwangalia, mtu aliye mnyonge, mwenye roho iliyopondeka, atetemekaye asikiapo neno langu.
Lakini wewe, Ee Danieli, yafunge maneno haya, ukakitie mhuri kitabu, hata wakati wa mwisho; wengi wataenda mbio huku na huko, na maarifa yataongezeka.
Mtafuteni BWANA, enyi nyote mlio wanyenyekevu wa dunia, ninyi mliozitenda hukumu zake; itafuteni haki, utafuteni unyenyekevu; huenda mtafichwa katika siku ya hasira ya BWANA.
Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;
vipofu wanapata kuona, viwete wanakwenda, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini wanahubiriwa Habari Njema.
Kwa hiyo wekeeni mbali uchafu wote na ubaya uzidio, na kupokea kwa upole neno lile lililopandwa ndani, liwezalo kuziokoa roho zenu.
Ndugu zangu wapenzi, sikilizeni, Je! Mungu hakuwachagua maskini wa dunia wawe matajiri wa imani na warithi wa ufalme aliowaahidia wampendao?