Isaya 29:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Je! Si muda mdogo uliobaki, na Lebanoni itageuzwa kuwa shamba lizaalo sana, na lile shamba lizaalo sana litahesabiwa kuwa msitu? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Bado kidogo tu, msitu wa Lebanoni utageuzwa kuwa shamba lenye rutuba, na shamba lenye rutuba kuwa msitu. Biblia Habari Njema - BHND Bado kidogo tu, msitu wa Lebanoni utageuzwa kuwa shamba lenye rutuba, na shamba lenye rutuba kuwa msitu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Bado kidogo tu, msitu wa Lebanoni utageuzwa kuwa shamba lenye rutuba, na shamba lenye rutuba kuwa msitu. Neno: Bibilia Takatifu Kwa muda mfupi sana, je, Lebanoni haitageuzwa kuwa shamba lenye rutuba, na shamba lenye rutuba liwe kama msitu? Neno: Maandiko Matakatifu Kwa muda mfupi sana, je, Lebanoni haitageuzwa kuwa shamba lenye rutuba, na shamba lenye rutuba liwe kama msitu? BIBLIA KISWAHILI Je! Si muda mdogo uliobaki, na Lebanoni itageuzwa kuwa shamba lizaalo sana, na lile shamba lizaalo sana litahesabiwa kuwa msitu? |
Wapitapo katika bonde la baraka, Hulifanya kuwa chemchemi, Naam, mvua ya vuli hulijaza baraka.
hata roho itakapomwagwa juu yetu kutoka juu; hata jangwa litakapokuwa shamba lizaalo sana; nalo shamba lizaalo sana litakapohesabiwa kuwa msitu.
Nitapanda katika jangwa mwerezi, mshita, mhadasi, na mbono; nitatia katika nyika mberoshi, mtidhari, na mteashuri pamoja;
nami nitaliharibu; wala halitapogolewa wala kulimwa, bali litamea mbigili na miiba; nami nitayaamuru mawingu yasinyeshe mvua juu yake.
Badala ya michongoma utamea msonobari, Na badala ya mibigili, mhadesi; Jambo hili litakuwa la kumpatia BWANA jina, Litakuwa ishara ya milele isiyokatiliwa mbali.
Watu wako watakatifu waliumiliki kwa kitambo tu; adui zetu wamepakanyaga patakatifu pako.
Kwa maana wana wa Israeli watakaa siku nyingi bila mfalme, wala mtu mkuu, wala sadaka, wala nguzo, wala naivera, wala kinyago;
Basi, kwa ajili yenu, Sayuni utalimwa kama shamba lilimwavyo, na Yerusalemu utakuwa magofu; na mlima wa nyumba utakuwa kama mahali palipoinuka msituni.
Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapokawia, ingojee; kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia.
Kwa maana BWANA wa majeshi asema hivi, Kwa mara nyingine, kitambo kidogo tu, nitazitikisa hizo mbingu, na hii nchi, na bahari, na nchi kavu;
Kwa sababu hiyo nawaambia, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, nao watapewa taifa lingine lenye kuzaa matunda yake.