Yeye Mwenyezi hamwezi kumwona; Yeye ni mkuu mwenye uweza; Tena mwenye hukumu, na mwingi wa haki, hataonea.
Isaya 28:29 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Hayo nayo yatoka kwa BWANA wa majeshi, mwenye shauri la ajabu, apitaye wote kwa hekima yake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ujuzi huu nao watoka kwa Mwenyezi-Mungu wa majeshi. Mipango yake Mungu ni ya ajabu, hekima yake ni kamilifu kabisa. Biblia Habari Njema - BHND Ujuzi huu nao watoka kwa Mwenyezi-Mungu wa majeshi. Mipango yake Mungu ni ya ajabu, hekima yake ni kamilifu kabisa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ujuzi huu nao watoka kwa Mwenyezi-Mungu wa majeshi. Mipango yake Mungu ni ya ajabu, hekima yake ni kamilifu kabisa. Neno: Bibilia Takatifu Haya yote pia hutoka kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, mwenye mashauri ya ajabu, na anayepita wote kwa hekima. Neno: Maandiko Matakatifu Haya yote pia hutoka kwa bwana Mwenye Nguvu Zote, mwenye mashauri ya ajabu, na anayepita wote kwa hekima. BIBLIA KISWAHILI Hayo nayo yatoka kwa BWANA wa majeshi, mwenye shauri la ajabu, apitaye wote kwa hekima yake. |
Yeye Mwenyezi hamwezi kumwona; Yeye ni mkuu mwenye uweza; Tena mwenye hukumu, na mwingi wa haki, hataonea.
Ee BWANA, Mungu wangu, umefanya kwa wingi Miujiza yako na mawazo yako kwetu; Hakuna awezaye kufananishwa nawe; Kama ningependa kuyatangaza na kuyahubiri, Ni mengi sana hayahesabiki.
Ngano ya mkate husagwa; kwa maana haipuri siku zote bila kukoma; na ingawa gurudumu la gari lake na farasi wake huitawanya ngano ile, haisagi.
Lakini yeye naye ana akili, naye ataleta uovu, wala hatayatangua maneno yake; bali ataondoka juu ya nyumba yao watendao mabaya, na juu ya msaada wa hao watendao maovu.
ili waone, na kujua, wakafikiri, na kufahamu pamoja, ya kuwa mkono wa BWANA ndio uliofanya jambo hilo. Mtakatifu wa Israeli ndiye aliyeliumba.
Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto wa kiume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa Ajabu, Mungu Mwenye Nguvu, Baba wa Milele, Mfalme wa Amani.
mkuu wa mashauri, muweza katika kutenda; ambaye macho yake yamefumbuka juu ya njia zote za wanadamu, kumpa kila mtu kwa kadiri ya njia zake, na kwa kadiri ya matunda ya matendo yake,
Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mungu! Hukumu zake hazichunguziki, wala njia zake hazieleweki!