Isaya 28:26 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kwa maana Mungu wake anamwagiza vizuri na kumfundisha. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mtu huyo huwa anajua la kufanya, kwa sababu Mungu wake humfundisha. Biblia Habari Njema - BHND Mtu huyo huwa anajua la kufanya, kwa sababu Mungu wake humfundisha. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mtu huyo huwa anajua la kufanya, kwa sababu Mungu wake humfundisha. Neno: Bibilia Takatifu Mungu wake humwelekeza na kumfundisha njia iliyo sahihi. Neno: Maandiko Matakatifu Mungu wake humwelekeza na kumfundisha njia iliyo sahihi. BIBLIA KISWAHILI Kwa maana Mungu wake anamwagiza vizuri na kumfundisha. |
Atufundishaye zaidi ya wanyama wa nchi, Na kutufanya wenye hekima kuliko ndege wa angani?
Na ahimidiwe BWANA, mwamba wangu, Aifundishaye mikono yangu vita, Na vidole vyangu kupigana.
Nawe utawaambia watu wote wenye uwezo wa hali ya juu, niliowapa ubingwa wamfanyie Haruni mavazi ili awekwe wakfu anitumikie katika kazi ya ukuhani.
Basi Musa akawaita Bezaleli na Oholiabu, na kila mtu aliyekuwa na moyo wa akili, ambaye BWANA alimtia moyoni mwake hekima, kila mtu ambaye moyo wake ulimhimiza ili aende kuifanya kazi hiyo;
Akiisha kuulainisha uso wa nchi yake, je! Hamwagi huku na huko kunde, na kutupatupa jira, na kuitia ngano safu safu, na shayiri mahali pake palipochaguliwa, na kusemethi karibu na mipaka yake?
Kwa maana kunde zile hazipurwi kwa chombo kikali, wala gurudumu la gari halipitishwi huku na huko juu ya jira ile, bali kunde zile hupurwa kwa fimbo, na jira ile kwa ufito.
Atamfundisha nani maarifa? Atamfahamisha nani habari hii? Je! Ni wale walioachishwa maziwa, walioondolewa matitini?
Basi, kwa habari za hao vijana wanne, Mungu aliwapa maarifa na ujuzi katika elimu na hekima; Danieli naye alikuwa na ufahamu katika maono yote, na ndoto.
Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeukageuka.