Wakati wa kuzaliwa, na wakati wa kufa; Wakati wa kupanda, na wakati wa kung'oa kilichopandwa;
Isaya 28:24 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Je! Mwenye kulima alima daima, ili apande? Afunua daima madongoa ya nchi yake, na kuyavunja? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Je, alimaye ili kupanda hulima tu? Je, huendelea kulima na kusawazisha shamba lake? Biblia Habari Njema - BHND Je, alimaye ili kupanda hulima tu? Je, huendelea kulima na kusawazisha shamba lake? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Je, alimaye ili kupanda hulima tu? Je, huendelea kulima na kusawazisha shamba lake? Neno: Bibilia Takatifu Mkulima anapolima ili apande, je, hulima siku zote? Je, huendelea kubomoa ardhi na kusawazisha udongo? Neno: Maandiko Matakatifu Wakati mkulima alimapo ili apande, je, hulima siku zote? Je, huendelea kubomoa ardhi na kusawazisha udongo? BIBLIA KISWAHILI Je! Mwenye kulima alima daima, ili apande? Afunua daima madongoa ya nchi yake, na kuyavunja? |
Wakati wa kuzaliwa, na wakati wa kufa; Wakati wa kupanda, na wakati wa kung'oa kilichopandwa;
Akiisha kuulainisha uso wa nchi yake, je! Hamwagi huku na huko kunde, na kutupatupa jira, na kuitia ngano safu safu, na shayiri mahali pake palipochaguliwa, na kusemethi karibu na mipaka yake?
Maana BWANA awaambia hivi watu wa Yuda na Yerusalemu Ulimeni udongo katika konde zenu, wala msipande mbegu kati ya miiba.