Isaya 28:23 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Tegeni masikio, sikieni sauti yangu, sikilizeni mkasikie neno langu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Tegeni sikio msikilize ninayowaambieni; sikilizeni kwa makini hotuba yangu. Biblia Habari Njema - BHND Tegeni sikio msikilize ninayowaambieni; sikilizeni kwa makini hotuba yangu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Tegeni sikio msikilize ninayowaambieni; sikilizeni kwa makini hotuba yangu. Neno: Bibilia Takatifu Sikilizeni msikie sauti yangu, tegeni masikio na msikie niyasemayo. Neno: Maandiko Matakatifu Sikilizeni msikie sauti yangu, tegeni masikio na msikie niyasemayo. BIBLIA KISWAHILI Tegeni masikio, sikieni sauti yangu, sikilizeni mkasikie neno langu. |
Sikieni, enyi mbingu, tega sikio, Ee nchi, kwa maana BWANA amenena; Nimewalisha watoto na kuwalea, nao wameniasi.
Basi sasa msiwe watu wenye kudharau, vifungo vyenu msije vikakazwa; maana nimesikia kwa Bwana, BWANA wa majeshi, habari ya hukumu itakayotimizwa, nayo imekusudiwa, itakayoipata dunia yote pia.
Je! Mwenye kulima alima daima, ili apande? Afunua daima madongoa ya nchi yake, na kuyavunja?
Inukeni, enyi wanawake mnaostarehe, isikieni sauti yangu; enyi binti za watu msiojali, tegeni masikio yenu msikie maneno yangu.
Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho anayaambia makanisa. Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pili.
Lakini ninayo maneno machache juu yako, kwa kuwa unao huko watu washikao mafundisho ya Balaamu, yeye aliyemfundisha Balaki atie kikwazo mbele ya Waisraeli, kwamba wavile vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na kuzini.
Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho anayaambia makanisa. Yeye ashindaye, nitampa kula matunda ya mti wa uzima, ulio katika bustani ya Mungu.