Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

Isaya 25:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Kama vile joto katika mahali pakavu Utaushusha mshindo wa wageni; Kama ilivyo joto kwa kivuli cha wingu, Wimbo wa hao watishao utashushwa.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

ni kama joto la jua juu ya nchi kavu. Lakini wewe wakomesha fujo ya wageni. Kama wingu lizimavyo joto la jua ndivyo ukomeshavyo nyumba za ushindi za wakatili.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

ni kama joto la jua juu ya nchi kavu. Lakini wewe wakomesha fujo ya wageni. Kama wingu lizimavyo joto la jua ndivyo ukomeshavyo nyumba za ushindi za wakatili.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

ni kama joto la jua juu ya nchi kavu. Lakini wewe wakomesha fujo ya wageni. Kama wingu lizimavyo joto la jua ndivyo ukomeshavyo nyumba za ushindi za wakatili.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

na kama joto la jangwani. Wewe wanyamazisha kelele ya wageni; kama vile hari ipunguzwavyo na kivuli cha wingu, ndivyo wimbo wa wakatili unyamazishwavyo.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

na kama joto la jangwani. Wewe wanyamazisha makelele ya wageni; kama vile hari ipunguzwavyo na kivuli cha wingu, ndivyo wimbo wa wakatili unyamazishwavyo.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Kama vile joto katika mahali pakavu Utaushusha mshindo wa wageni; Kama ilivyo joto kwa kivuli cha wingu, Wimbo wa hao watishao utashushwa.

Tazama sura
Tafsiri zingine

Isaya 25:5
27 Marejeleo ya Msalaba  

Alitandaza wingu liwe kifuniko, Na moto ili uwaangazie usiku.

Nami nitaadhibu ulimwengu kwa sababu ya ubaya wake, na wenye dhambi kwa sababu ya hatia yao; nami nitaikomesha fahari yao wenye kiburi; nami nitayashusha chini majivuno yao walio wakali;

Bali wewe umetupwa mbali na kaburi lako, Kama chipukizi lililochukiza kabisa; Kama vazi la wale waliouawa, Wale waliochomwa kwa upanga, Wale washukao mpaka misingi ya shimo; Kama mzoga uliokanyagwa chini ya miguu.

Maana BWANA ameniambia hivi, Mimi nitatulia, na kuangalia katika makazi yangu, kama wakati wa mwangaza mweupe wa jua kali, mfano wa wingu la umande katika joto la mavuno.

Na katika mlima huu BWANA wa majeshi atawafanyia mataifa yote karamu ya vitu vinono, karamu ya divai iliyokaa juu ya urojorojo wake, karamu ya vinono vilivyojaa mafuta, karamu ya divai iliyokaa juu ya urojorojo wake, iliyochujwa sana.

Hawataona njaa, wala hawataona kiu; joto halitawapiga, wala jua; kwa maana yeye aliyewarehemu atawatangulia, naam, karibu na chemchemi za maji atawaongoza.

Nawe utapaa juu, utakuja kama tufani, utakuwa kama wingu kuifunika nchi, wewe, na vikosi vyako vyote, na kabila nyingi za watu pamoja nawe.