Isaya 23:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ni nani aliyefanya shauri hili juu ya Tiro, uliotia watu mataji, ambao wafanya biashara wake walikuwa wana wa wafalme, na wachuuzi wake ni watu wakuu wa dunia? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ni nani aliyepanga mambo haya dhidi ya Tiro, mji uliowatawaza wafalme, wafanyabiashara wake walikuwa wakuu, wakaheshimiwa duniani kote? Biblia Habari Njema - BHND Ni nani aliyepanga mambo haya dhidi ya Tiro, mji uliowatawaza wafalme, wafanyabiashara wake walikuwa wakuu, wakaheshimiwa duniani kote? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ni nani aliyepanga mambo haya dhidi ya Tiro, mji uliowatawaza wafalme, wafanyabiashara wake walikuwa wakuu, wakaheshimiwa duniani kote? Neno: Bibilia Takatifu Ni nani amepanga hili dhidi ya Tiro, mji utoao mataji, ambao wafanyabiashara wake ni wana wa mfalme na wachuuzi wake ni watu mashuhuri wa dunia? Neno: Maandiko Matakatifu Ni nani amepanga hili dhidi ya Tiro, mji utoao mataji, ambao wafanyabiashara wake ni wana wa mfalme na wachuuzi wake ni watu mashuhuri wa dunia? BIBLIA KISWAHILI Ni nani aliyefanya shauri hili juu ya Tiro, uliotia watu mataji, ambao wafanya biashara wake walikuwa wana wa wafalme, na wachuuzi wake ni watu wakuu wa dunia? |
Wawezaje, basi, kurudisha nyuma uso wa afisa mmoja wa watumishi walio wadogo wa bwana wangu, na kuitumainia Misri upewe magari na farasi?
Nao wataufanya utajiri wako kuwa mateka, na bidhaa yako kuwa mawindo; nao watazibomoa kuta zako, na kuziharibu nyumba zako zipendezazo; nao watatupa mawe yako, na miti yako, na mavumbi yako, kati ya maji.
Umeongeza wafanya biashara wako kuwa wengi kuliko nyota za mbinguni; tunutu huharibu; kisha huruka juu na kwenda zake.
Na Tiro alijijengea ngome, akakusanya fedha kama mchanga, dhahabu safi kama matope ya njia kuu.
wala nuru ya taa haitamulika ndani yako tena kabisa; wala sauti ya bwana arusi na bibi arusi haitasikika ndani yako tena kabisa; maana hao wafanya biashara wako walikuwa wakuu wa nchi, kwa kuwa mataifa yote walidanganywa kwa uchawi wako.
Kwa sababu hiyo mapigo yake yatakuja katika siku moja, mauti, na huzuni, na njaa, naye atateketezwa kabisa kwa moto. Kwa maana Bwana Mungu aliyemhukumu ni mwenye nguvu.