Mimi nimeona watumwa wamepanda farasi, na wakuu wakienda kwa miguu juu ya nchi kama watumwa.
Isaya 23:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Je! Huu ndio mji wenu wa furaha, ambao mwanzo wake ulikuwako tangu siku za kale, ambao miguu yake ilimchukua akae mbali sana? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Je, huu ndio mji wa furaha wa Tiro, mji ambao ulijengwa zamani za kale, ambao wakazi wake walikwenda kumiliki nchi za mbali? Biblia Habari Njema - BHND Je, huu ndio mji wa furaha wa Tiro, mji ambao ulijengwa zamani za kale, ambao wakazi wake walikwenda kumiliki nchi za mbali? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Je, huu ndio mji wa furaha wa Tiro, mji ambao ulijengwa zamani za kale, ambao wakazi wake walikwenda kumiliki nchi za mbali? Neno: Bibilia Takatifu Je, huu ndio mji wenu uliojaa sherehe, mji wa zamani, zamani kabisa ambao miguu yake imeuchukua kufanya makao nchi za mbali sana? Neno: Maandiko Matakatifu Je, huu ndio mji wenu uliojaa sherehe, mji wa zamani, zamani kabisa ambao miguu yake imeuchukua kufanya makao nchi za mbali sana? BIBLIA KISWAHILI Je! Huu ndio mji wenu wa furaha, ambao mwanzo wake ulikuwako tangu siku za kale, ambao miguu yake ilimchukua akae mbali sana? |
Mimi nimeona watumwa wamepanda farasi, na wakuu wakienda kwa miguu juu ya nchi kama watumwa.
Ewe uliyejaa makelele, Mji wa ghasia, mji wenye furaha; Watu wako waliouawa hawakuuawa kwa upanga, Wala hawakufa vitani.
Juu ya nchi ya watu wangu itamea michongoma na mibigili; naam, juu ya nyumba za furaha katika mji ulio na shangwe;
kisha mpaka ulizunguka kuelekea Rama, na mji wa Tiro ulio na boma; kisha mpaka ulizunguka kuelekea Hosa; na matokeo yake yalikuwa baharini katika nchi ya Akzibu;