Basi, itakuwa katika siku ile, Tiro utasahauliwa miaka sabini, kadiri ya siku za mfalme mmoja; hata mwisho wa miaka sabini, Tiro utakuwa kama vile ulivyo wimbo wa kahaba.
Isaya 23:16 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Twaa kinubi, tembea mjini, Ewe kahaba uliyesahauliwa; Piga vizuri, imba nyimbo nyingi, Upate kukumbukwa tena. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Twaa kinubi chako uzungukezunguke mjini, ewe malaya uliyesahaulika! Imba nyimbo tamutamu. Imba nyimbo nyinginyingi ili upate kukumbukwa tena.” Biblia Habari Njema - BHND “Twaa kinubi chako uzungukezunguke mjini, ewe malaya uliyesahaulika! Imba nyimbo tamutamu. Imba nyimbo nyinginyingi ili upate kukumbukwa tena.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Twaa kinubi chako uzungukezunguke mjini, ewe malaya uliyesahaulika! Imba nyimbo tamutamu. Imba nyimbo nyinginyingi ili upate kukumbukwa tena.” Neno: Bibilia Takatifu “Twaa kinubi, tembea mjini kote, ewe kahaba uliyesahauliwa; piga kinubi vizuri, imba nyimbo nyingi, ili upate kukumbukwa.” Neno: Maandiko Matakatifu “Twaa kinubi, tembea mjini kote, ewe kahaba uliyesahauliwa; piga kinubi vizuri, imba nyimbo nyingi, ili upate kukumbukwa.” BIBLIA KISWAHILI Twaa kinubi, tembea mjini, Ewe kahaba uliyesahauliwa; Piga vizuri, imba nyimbo nyingi, Upate kukumbukwa tena. |
Basi, itakuwa katika siku ile, Tiro utasahauliwa miaka sabini, kadiri ya siku za mfalme mmoja; hata mwisho wa miaka sabini, Tiro utakuwa kama vile ulivyo wimbo wa kahaba.
Hata itakuwa mwisho wa miaka sabini, BWANA ataizuru nchi ya Tiro, naye atarudi apate ujira wake, atafanya ukahaba pamoja na falme zote za ulimwengu juu ya uso wa dunia.
Wote wakupendao wamekusahau; hawakutafuti; maana nimekujeruhi kwa jeraha la adui, kwa adhabu ya mtu mkatili; kwa sababu ya ukubwa wa uovu wako, kwa sababu dhambi zako zilikuwa zimeongezeka.
Kwa sababu ya wingi wa ukahaba wa yule kahaba mzuri, yule bibi wa mambo ya uchawi, auzaye mataifa kwa ukahaba wake, na jamaa za watu kwa uchawi wake.