Na walipokwisha kumwita mfalme, wakatokewa na Eliakimu, mwana wa Hilkia, aliyekuwa msimamizi wa nyumba ya mfalme, na Shebna, mwandishi, na Yoa, mwana wa Asafu, mwenye kuandika tarehe.
Isaya 22:20 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na itakuwa katika siku ile nitamwita mtumishi wangu Eliakimu, mwana wa Hilkia; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Siku hiyo, nitamleta mtumishi wangu Eliakimu mwana wa Hilkia. Biblia Habari Njema - BHND “Siku hiyo, nitamleta mtumishi wangu Eliakimu mwana wa Hilkia. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Siku hiyo, nitamleta mtumishi wangu Eliakimu mwana wa Hilkia. Neno: Bibilia Takatifu “Katika siku ile, nitamwita mtumishi wangu, Eliakimu mwana wa Hilkia. Neno: Maandiko Matakatifu “Katika siku ile, nitamwita mtumishi wangu, Eliakimu mwana wa Hilkia. BIBLIA KISWAHILI Na itakuwa katika siku ile nitamwita mtumishi wangu Eliakimu, mwana wa Hilkia; |
Na walipokwisha kumwita mfalme, wakatokewa na Eliakimu, mwana wa Hilkia, aliyekuwa msimamizi wa nyumba ya mfalme, na Shebna, mwandishi, na Yoa, mwana wa Asafu, mwenye kuandika tarehe.
Ndipo Eliakimu, mwana wa Hilkia, aliyekuwa msimamizi wa nyumba ya mfalme, na Shebna, mwandishi, na Yoa, mwana wa Asafu, mwenye kuandika tarehe, wakaenda kwa Hezekia, na nguo zao zimeraruliwa, wakamwambia maneno ya yule kamanda.
Ndipo Eliakimu, mwana wa Hilkia, na Shebna, na Yoa, wakamwambia yule kamanda, Tafadhali, sema na watumishi wako kwa lugha ya Kiashuri; maana tunaifahamu; wala usiseme nasi kwa lugha ya Kiyahudi, masikioni mwa watu wote walio ukutani.
Ndipo Eliakimu, mwana wa Hilkia, aliyekuwa msimamizi wa nyumba ya mfalme, na Shebna, mwandishi, na Yoa, mwana wa Asafu mwenye kuandika kumbukumbu, wakaenda kwa Hezekia, na nguo zao zikiwa zimeraruliwa, wakamwambia Hezekia maneno ya yule kamanda.
Wakamtokea Eliakimu, mwana wa Hilkia, aliyekuwa msimamizi wa nyumba ya mfalme, na Shebna, mwandishi, na Yoa, mwana wa Asafu, mwenye kuandika kumbukumbu.
Akamtuma Eliakimu aliyekuwa msimamizi wa nyumba yake na Shebna, mwandishi, na wazee wa makuhani, wakiwa wamejivika nguo za magunia, waende kwa Isaya nabii, mwana wa Amozi.