Isaya 19:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na vijito vya mto vitatoa uvundo, na mifereji ya Misri itakuwa haina maji mengi, itakauka; manyasi na mianzi itanyauka. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mifereji yake itatoa uvundo, vijito vyake vitapunguka na kukauka. Nyasi na mafunjo yake yataoza. Biblia Habari Njema - BHND Mifereji yake itatoa uvundo, vijito vyake vitapunguka na kukauka. Nyasi na mafunjo yake yataoza. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mifereji yake itatoa uvundo, vijito vyake vitapunguka na kukauka. Nyasi na mafunjo yake yataoza. Neno: Bibilia Takatifu Mifereji itanuka; vijito vya Misri vitapungua na kukauka. Matete na nyasi vitanyauka, Neno: Maandiko Matakatifu Mifereji itanuka; vijito vya Misri vitapungua na kukauka. Mafunjo na nyasi vitanyauka, BIBLIA KISWAHILI Na vijito vya mto vitatoa uvundo, na mifereji ya Misri itakuwa haina maji mengi, itakauka; manyasi na mianzi itanyauka. |
Nimechimba na kunywa maji mageni, na kwa nyayo za miguu yangu nitaikausha mito yote ya Misri.
Na alipokuwa hawezi kumficha tena, akamtengenezea kikapu cha mafunjo akakitaliza kwa sifa na lami, akamtia mtoto ndani yake, akakiweka kwenye nyasi kando ya mto.
Na hao samaki walio mtoni watakufa, na huo mto utatoa uvundo; nao Wamisri watachukizwa kuyanywa maji ya mtoni.
Kwa maana maji ya Nimrimu yamekuwa mahali palipoharibika, kwa kuwa majani yamekauka, miche imenyauka, majani mabichi yamekoma.
Ipelekayo wajumbe wake kwa njia ya bahari, Na katika vyombo vya manyasi juu ya maji. Nendeni, wajumbe wepesi, kwa watu warefu, laini; Watu watishao tangu mwanzo wao hata sasa; Taifa la wenye nguvu, wakanyagao watu, Ambao mito inakata nchi yao.
Je! Wewe u mwema kuliko No-amoni, uliowekwa kati ya mito, uliozungukwa na maji; ambao boma lake lilikuwa bahari, na bahari ilikuwa ukuta wake.