Isaya 19:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Wakuu wa Soani wamekuwa wapumbavu kabisa; washauri wenye hekima wa Farao, ushauri wao umepumbazika; mwawezaje kumwambia Farao, Mimi ni mwana wa wenye hekima, ni mwana wa wafalme wa zamani? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Viongozi wa mji wa Soani ni wapumbavu kabisa, washauri wa Farao wanatoa shauri la kijinga! Awezaje kila mmoja kumwambia Farao, “Mimi ni mzawa wa mtaalamu stadi; mzawa wa wafalme wa hapo kale!” Biblia Habari Njema - BHND Viongozi wa mji wa Soani ni wapumbavu kabisa, washauri wa Farao wanatoa shauri la kijinga! Awezaje kila mmoja kumwambia Farao, “Mimi ni mzawa wa mtaalamu stadi; mzawa wa wafalme wa hapo kale!” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Viongozi wa mji wa Soani ni wapumbavu kabisa, washauri wa Farao wanatoa shauri la kijinga! Awezaje kila mmoja kumwambia Farao, “Mimi ni mzawa wa mtaalamu stadi; mzawa wa wafalme wa hapo kale!” Neno: Bibilia Takatifu Maafisa wa Soani ni wapumbavu kabisa, washauri wa Farao wenye busara wanatoa ushauri wa kijinga. Unawezaje kumwambia Farao, “Mimi ni mmoja wa watu wenye hekima, mwanafunzi wa wafalme wa zamani”? Neno: Maandiko Matakatifu Maafisa wa Soani ni wapumbavu kabisa, washauri wa Farao wenye busara wanatoa ushauri wa kijinga. Unawezaje kumwambia Farao, “Mimi ni mmojawapo wa watu wenye hekima, mwanafunzi wa wafalme wa zamani”? BIBLIA KISWAHILI Wakuu wa Soani wamekuwa wapumbavu kabisa; washauri wenye hekima wa Farao, ushauri wao umepumbazika; mwawezaje kumwambia Farao, Mimi ni mwana wa wenye hekima, ni mwana wa wafalme wa zamani? |
Yeye huwaondoa washauri wakiwa wamevuliwa nguo, Naye huwafanya waamuzi kuwa ni wapumbavu.
Kisha hao vyura watakwea juu yako wewe, na juu ya watu wako, na juu ya watumishi wako wote.
Wakuu wa Soani wamekuwa wapumbavu, wakuu wa Nofu wamedanganyika; na hao walio mawe ya pembeni ya kabila zake wameipotosha Misri.
Na roho yao Misri itaondolewa, nami nitaiharibu mipango yao, nao watakwenda kwa sanamu zao, na kwa waganga, na kwa wapiga ramli na kwa wachawi.
kwa sababu hiyo mimi nitafanya tena kazi ya ajabu kati ya watu hawa, kazi ya ajabu na mwujiza; na akili za watu wao wenye akili zitapotea, na ufahamu wa wenye busara wao utafichwa.
Nizitanguaye ishara za waongo, na kuwatia waganga wazimu; niwarudishaye nyuma wenye hekima, na kuyageuza maarifa yao kuwa ujinga;
Kila mtu amekuwa kama mnyama, hana maarifa; Kila mfua dhahabu amefedheheshwa na sanamu yake ya kuchonga; Maana sanamu yake ya kuyeyuka ni uongo, Wala hamna pumzi ndani yake.
Kwa sababu wachungaji wamekuwa kama wanyama, wala hawakuuliza kwa BWANA; basi hawakufanikiwa, na makundi yao yote yametawanyika.
Kuhusu Edomu. BWANA wa majeshi asema hivi, Je! Hakuna tena hekima katika Temani? Mashauri yamewapotea wenye busara? Je! Imetoweka hekima yao?
Wenye hekima wametahayari, wamefadhaika na kushikwa; tazama, wamelikataa neno la BWANA, wana akili gani ndani yao?
Moyo wako uliinuka kwa sababu ya uzuri wako; umeiharibu hekima yako kwa sababu ya mwangaza wako; nimekutupa chini, nimekulaza mbele ya wafalme, wapate kukutazama.
Nami nitaifanya Pathrosi kuwa ukiwa, nami nitatia moto katika Soani, nami nitatekeleza hukumu katika No.
Madhara yatakuja juu ya madhara, na habari ya shari juu ya habari ya shari; nao watakwenda kwa nabii kutaka maono; lakini hiyo sheria itampotea kuhani, na mashauri yatawapotea wazee.
Watu wote wa mapatano yako Wamekufukuza, hadi mipakani; Wale waliofanya amani nawe Wamekudanganya, na kukushinda; Walao mkate wako wameweka mtego chini yako; Wala hana ufahamu wa hayo ndani yake.
Siku hiyo, je! Sitawaangamiza watu wenye akili katika Edomu, na wenye ufahamu katika kilima cha Esau? Asema BWANA.
Wakapanda katika Negebu, wakafika Hebroni; na Ahimani, na Sheshai, na Talmai, wana wa Anaki, walikuwako huko. Nao Hebroni ulijengwa miaka saba kabla ya Soani wa Misri.