Isaya 19:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na nguzo za nchi zitavunjika vipande vipande, wote wafanyao kazi ya mshahara watahuzunika nafsini mwao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wafuma nguo watafedheheshwa, na vibarua watahuzunika. Biblia Habari Njema - BHND Wafuma nguo watafedheheshwa, na vibarua watahuzunika. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wafuma nguo watafedheheshwa, na vibarua watahuzunika. Neno: Bibilia Takatifu Wafanyao kazi ya kufuma nguo watahuzunishwa, nao vibarua wataugua moyoni. Neno: Maandiko Matakatifu Wafanyao kazi ya kufuma nguo watahuzunishwa, nao vibarua wataugua moyoni. BIBLIA KISWAHILI Na nguzo za nchi zitavunjika vipande vipande, wote wafanyao kazi ya mshahara watahuzunika nafsini mwao. |
BWANA akamwambia Musa, Mwambie Haruni, Shika fimbo yako, kaunyoshe mkono wako juu ya maji ya Misri, juu ya mito yao, juu ya vijito vyao, na juu ya maziwa ya maji yao, na juu ya visima vyao vyote vya maji, ili yageuke kuwa damu, nako kutakuwa na damu katika nchi yote ya Misri, katika vyombo vya mti, na katika vyombo vya jiwe.
BWANA akamwambia Musa, Mwambie Haruni, Nyosha mkono wako na fimbo yako juu ya mito, juu ya vijito, na juu ya maziwa ya maji, ukawalete vyura waje juu ya nchi yote ya Misri.
Kwa kuwa nchi mwingiayo kuimiliki, si mfano wa nchi ya Misri mlikotoka, uliyokuwa ukipanda mbegu zako humo na kuinyunyizia maji kwa mguu wako, kama shamba la mboga;