Isaya 14:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kuzimu chini kumetaharuki kwa ajili yako, Ili kukulaki utakapokuja; Huwaamsha waliokufa kwa ajili yako, Naam, walio wakuu wote wa dunia; Huwainua wafalme wote wa mataifa, Watoke katika viti vyao vya enzi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Kuzimu nako kumechangamka, ili kukulaki wakati utakapokuja. Kunaiamsha mizimu ije kukusalimu na wote waliokuwa wakuu wa dunia; huwaamsha kutoka viti vyao vya enzi wote waliokuwa wafalme wa mataifa. Biblia Habari Njema - BHND “Kuzimu nako kumechangamka, ili kukulaki wakati utakapokuja. Kunaiamsha mizimu ije kukusalimu na wote waliokuwa wakuu wa dunia; huwaamsha kutoka viti vyao vya enzi wote waliokuwa wafalme wa mataifa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Kuzimu nako kumechangamka, ili kukulaki wakati utakapokuja. Kunaiamsha mizimu ije kukusalimu na wote waliokuwa wakuu wa dunia; huwaamsha kutoka viti vyao vya enzi wote waliokuwa wafalme wa mataifa. Neno: Bibilia Takatifu Kuzimu kumetaharuki kukulaki unapokuja, kunaamsha roho za waliokufa ili kukupokea, wote waliokuwa viongozi katika ulimwengu, kunawafanya wainuke kwenye viti vyao vya kifalme: wale wote waliokuwa wafalme juu ya mataifa. Neno: Maandiko Matakatifu Kuzimu kote kumetaharuki kukulaki unapokuja, kunaamsha roho za waliokufa ili kukupokea, wote waliokuwa viongozi katika ulimwengu, kunawafanya wainuke kwenye viti vyao vya kifalme: wale wote waliokuwa wafalme juu ya mataifa. BIBLIA KISWAHILI Kuzimu chini kumetaharuki kwa ajili yako, Ili kukulaki utakapokuja; Huwaamsha waliokufa kwa ajili yako, Naam, walio wakuu wote wa dunia; Huwainua wafalme wote wa mataifa, Watoke katika viti vyao vya enzi. |
Kwa hiyo kuzimu kumeongeza tamaa yake, kumefunua kinywa chake bila kiasi; na utukufu wao, na wingi wao, na ghasia yao, naye pia afurahiye miongoni mwao, hushuka na kuingia humo.
Kimbieni kutoka kati ya Babeli, mkatoke katika nchi ya Wakaldayo, mkawe kama mabeberu mbele ya makundi.
ndipo nitakapokushusha pamoja nao washukao shimoni, uende kwa watu wa kale; nami nitakukalisha pande za chini za nchi; mahali palipokuwa ukiwa tangu zamani, pamoja nao washukao shimoni; ili usikaliwe na watu, wala usiweke utukufu wako katika nchi yao walio hai.