Kwa maana fimbo ya udhalimu Haitakaa juu ya nchi ya wenye haki; Ili wenye haki wasije wakainyosha Mikono yao kwenye upotovu.
Isaya 14:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC BWANA amelivunja gongo la wabaya, Fimbo ya enzi yao wenye kutawala. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenyezi-Mungu amelivunja gongo la waovu, ameivunja fimbo ya kifalme ya watawala, Biblia Habari Njema - BHND Mwenyezi-Mungu amelivunja gongo la waovu, ameivunja fimbo ya kifalme ya watawala, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenyezi-Mungu amelivunja gongo la waovu, ameivunja fimbo ya kifalme ya watawala, Neno: Bibilia Takatifu Mwenyezi Mungu amevunja fimbo ya mwovu, fimbo ya utawala ya watawala, Neno: Maandiko Matakatifu bwana amevunja fimbo ya mwovu, fimbo ya utawala ya watawala, BIBLIA KISWAHILI BWANA amelivunja gongo la wabaya, Fimbo ya enzi yao wenye kutawala. |
Kwa maana fimbo ya udhalimu Haitakaa juu ya nchi ya wenye haki; Ili wenye haki wasije wakainyosha Mikono yao kwenye upotovu.
Kama simba angurumaye, na dubu mwenye njaa; Ndivyo alivyo mtu mbaya awatawalaye maskini.
Ole wake Ashuru! Fimbo ya hasira yangu, ambaye gongo lililo mkononi mwake ni ghadhabu yangu!
Nami nitaadhibu ulimwengu kwa sababu ya ubaya wake, na wenye dhambi kwa sababu ya hatia yao; nami nitaikomesha fahari yao wenye kiburi; nami nitayashusha chini majivuno yao walio wakali;
Msifurahi, Enyi Wafilisti wote, Kwa sababu fimbo ile iliyokupiga imevunjika; Maana katika shina la nyoka atatoka fira, Na uzao wake ni joka la moto arukaye Sef 2:4-7; Zek 9:5-7
utatunga mithali hii juu ya mfalme wa Babeli, na kusema, Jinsi mdhalimu alivyokoma; Jinsi ulivyokoma mji ule wenye ujeuri!
Yeye aliyewapiga mataifa kwa ghadhabu, Kwa mapigo yasiyokoma; Aliyewatawala mataifa kwa hasira, Ameadhibiwa asizuie mtu.
Umeliongeza taifa, umezidisha furaha yao; Wanafurahi mbele zako, Kama furaha ya wakati wa mavuno, Kama watu wafurahivyo wagawanyapo nyara.
Kwa maana umeivunja nira ya mzigo wake, na gongo la bega lake, na fimbo yake yeye aliyemwonea, kama katika siku ya Midiani.
Wamesikia kwamba napiga kite; Hakuna hata mmoja wa kunifariji; Adui zangu wote wamesikia habari ya mashaka yaliyonipata; Hufurahi kwa kuwa umeyafanya hayo; Utaileta siku ile uliyoitangaza, Nao watakuwa kama mimi.