Ahazi akalala na babaze, akazikwa pamoja na babaze katika mji wa Daudi; na Hezekia mwanawe akatawala mahali pake.
Isaya 14:28 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ufunuo huu ulikuja mwaka ule alipokufa mfalme Ahazi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwaka alipofariki mfalme Ahazi, Mungu alitoa kauli hii: Biblia Habari Njema - BHND Mwaka alipofariki mfalme Ahazi, Mungu alitoa kauli hii: Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwaka alipofariki mfalme Ahazi, Mungu alitoa kauli hii: Neno: Bibilia Takatifu Neno hili lilikuja mwaka ule Mfalme Ahazi alipofariki: Neno: Maandiko Matakatifu Neno hili lilikuja mwaka ule Mfalme Ahazi alipofariki: BIBLIA KISWAHILI Ufunuo huu ulikuja mwaka ule alipokufa mfalme Ahazi. |
Ahazi akalala na babaze, akazikwa pamoja na babaze katika mji wa Daudi; na Hezekia mwanawe akatawala mahali pake.
Na katika kila mji wa Yuda akafanya mahali pa juu pa kuifukizia miungu mingine uvumba, akamkasirisha BWANA, Mungu wa babaze.
Ahazi akalala na babaze, wakamzika mjini, yaani, Yerusalemu; maana hawakumleta makaburini mwa wafalme wa Israeli; na Hezekia mwanawe akatawala mahali pake.
Katika mwaka ule aliokufa mfalme Uzia nilimwona Bwana ameketi katika kiti cha enzi, kilicho juu sana na kuinuliwa sana, na pindo za vazi lake zikalijaza hekalu.
Bwana MUNGU asema hivi; Kwa kuwa Wafilisti wametenda mambo kwa kujilipiza kisasi, nao wamejilipiza kisasi kwa moyo wa ujeuri, ili kupaangamiza kwa uadui wa daima;
Ashkeloni ataona haya na kuogopa; Gaza pia, naye atafadhaika sana; na Ekroni, kwa maana matarajio yake yatatahayarika; na mfalme ataangamia toka Gaza, na Ashkeloni atakuwa hana watu.