Wakaenda ili kumzika; lakini hawakuona kitu ila kifuvu cha kichwa chake, na miguu yake, na vitanga vya mikono yake.
Isaya 14:18 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Wafalme wote wa mataifa wamezikwa wote kwa heshima, Kila mmoja ndani ya nyumba yake mwenyewe; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wafalme wote wa mataifa wamezikwa kwa heshima kila mmoja ndani ya kaburi lake. Biblia Habari Njema - BHND Wafalme wote wa mataifa wamezikwa kwa heshima kila mmoja ndani ya kaburi lake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wafalme wote wa mataifa wamezikwa kwa heshima kila mmoja ndani ya kaburi lake. Neno: Bibilia Takatifu Wafalme wote wa mataifa wamelala kwa heshima kila mmoja katika kaburi lake. Neno: Maandiko Matakatifu Wafalme wote wa mataifa wamelala kwa heshima kila mmoja katika kaburi lake. BIBLIA KISWAHILI Wafalme wote wa mataifa wamezikwa wote kwa heshima, Kila mmoja ndani ya nyumba yake mwenyewe; |
Wakaenda ili kumzika; lakini hawakuona kitu ila kifuvu cha kichwa chake, na miguu yake, na vitanga vya mikono yake.
Wakamzika katika mji wa Daudi kati ya wafalme, kwa sababu ametenda mema katika Israeli, na kwa Mungu, na katika nyumba yake.
Hata walipoondoka kwake, (nao walimwacha ameshikwa sana na maradhi,) watumishi wake mwenyewe wakamfanyia fitina kwa ajili ya damu ya mwana wa Yehoyada kuhani, wakamwua kitandani pake, akafa; wakamzika mjini mwa Daudi, lakini hawakumzika katika makaburi ya wafalme.
Kwani najua kuwa utanileta hata kifoni, Niifikie nyumba waliyoaandaliwa wenye uhai wote.
Naam, wataogopa kilichoinuka Na vitisho vitakuwapo njiani; Na mlozi utachanua maua; Na panzi atakuwa ni mzigo mzito; Na pilipili hoho itapasuka; Maana mtu aiendea nyumba yake ya milele, Nao waombolezao wazunguka njiani.
Mtu akizaa watoto mia moja, akaishi miaka mingi, hata siku za maisha yake zikiwa nyingi, lakini nafsi yake haikushiba mema; tena ikiwa, zaidi ya hayo, amekosa maziko; mimi nasema, Heri mimba iliyoharibika kuliko huyo;
Aliyeufanya ulimwengu ukiwa, akaipindua miji yake; Asiyewafungua wafungwa wake waende kwao?
Bali wewe umetupwa mbali na kaburi lako, Kama chipukizi lililochukiza kabisa; Kama vazi la wale waliouawa, Wale waliochomwa kwa upanga, Wale washukao mpaka misingi ya shimo; Kama mzoga uliokanyagwa chini ya miguu.
Unafanyaje hapa? Nawe una nani hapa? Hata ukachimba kaburi hapa; ukamchimbia kaburi huko juu, na kumchongea makao katika jabali!