Wao wakuonao watakukazia macho, Watakuangalia sana, wakisema, Je! Huyu ndiye aliyeitetemesha dunia, Huyu ndiye aliyetikisa falme;
Isaya 14:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Aliyeufanya ulimwengu ukiwa, akaipindua miji yake; Asiyewafungua wafungwa wake waende kwao? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema aliyegeuza dunia kuwa kama jangwa, akaangamiza miji yake, na kuwanyima wafungwa wake kurudi kwao?’ Biblia Habari Njema - BHND aliyegeuza dunia kuwa kama jangwa, akaangamiza miji yake, na kuwanyima wafungwa wake kurudi kwao?’ Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza aliyegeuza dunia kuwa kama jangwa, akaangamiza miji yake, na kuwanyima wafungwa wake kurudi kwao?’ Neno: Bibilia Takatifu yule aliyeifanya dunia kuwa jangwa, aliyeipindua miji yake, na ambaye hakuwaachia mateka wake waende nyumbani?” Neno: Maandiko Matakatifu yule aliyeifanya dunia kuwa jangwa, aliyeipindua miji yake, na ambaye hakuwaachia mateka wake waende nyumbani?” BIBLIA KISWAHILI Aliyeufanya ulimwengu ukiwa, akaipindua miji yake; Asiyewafungua wafungwa wake waende kwao? |
Wao wakuonao watakukazia macho, Watakuangalia sana, wakisema, Je! Huyu ndiye aliyeitetemesha dunia, Huyu ndiye aliyetikisa falme;
Wafalme wote wa mataifa wamezikwa wote kwa heshima, Kila mmoja ndani ya nyumba yake mwenyewe;
Mimi nimemwinua katika haki, nami nitazinyosha njia zake zote; ataujenga mji wangu, naye atawaacha huru watu wangu waliohamishwa, si kwa kulipwa fedha, wala kwa kupewa zawadi, asema BWANA wa majeshi.
Je! Saumu niliyoichagua, siyo ya namna hii? Kufungua vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila nira?
BWANA wa majeshi asema hivi, Wana wa Israeli, na wana wa Yuda wameonewa sana, na pia wana wa Yuda vivyo hivyo, watekaji wao wote wamewashikilia sana; na wamekataa kuwaachilia waondoke.
ambao makaburi yao yamewekwa pande za shimo zilizo mbali sana, umati wote wamezunguka kaburi lake; wote pia wameuawa, wameanguka kwa upanga, waliotisha katika nchi yao walio hai.
Nami nitanyosha mkono wangu juu yao, na kuifanya nchi kuwa maganjo, tena ukiwa mbaya kuliko jangwa upande wa Dibla, katika makao yao yote; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.
Moto unaunguza vikali mbele yao; na nyuma yao miali ya moto inateketeza; hiyo nchi inafanana na bustani ya Edeni mbele yao, na nyuma yao imekuwa jangwa tupu; naam, hakuna aliyeokoka asipatikane nao.
Hao ni watu wa kutisha sana, wa kuogofya sana; hukumu yao na ukuu wao hutoka katika nafsi zao wenyewe.