Isaya 11:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na haki itakuwa mshipi wa viuno vyake, na uaminifu mshipi wa kujifungia. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Haki itakuwa kama mkanda wa kujifunga, uaminifu utakaa naye kama mkanda kiunoni. Biblia Habari Njema - BHND Haki itakuwa kama mkanda wa kujifunga, uaminifu utakaa naye kama mkanda kiunoni. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Haki itakuwa kama mkanda wa kujifunga, uaminifu utakaa naye kama mkanda kiunoni. Neno: Bibilia Takatifu Haki itakuwa mkanda wake na uaminifu utakuwa mshipi kiunoni mwake. Neno: Maandiko Matakatifu Haki itakuwa mkanda wake na uaminifu utakuwa mshipi kiunoni mwake. BIBLIA KISWAHILI Na haki itakuwa mshipi wa viuno vyake, na uaminifu mshipi wa kujifungia. |
Katika fahari yako usitawi uendelee Kwa ajili ya kweli, upole na haki Na mkono wako wa kulia Utakutendea mambo ya ajabu.
BWANA ametamalaki, amejivika adhama, BWANA amejivika, ukuu na nguvu, kama mavazi ya kifalme. Naam, ulimwengu umethibitika usitikisike;
Ee BWANA, wewe u Mungu wangu; Nitakutukuza na kulihimidi jina lako; Kwa kuwa umetenda mambo ya ajabu, Mashauri ya kale, kwa uaminifu na kweli.
Akajivika haki kama deraya kifuani, na chapeo cha wokovu kichwani pake, akajivika mavazi ya kisasi yawe mavazi yake, naye alivikwa wivu kama joho.
Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto wa kiume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa Ajabu, Mungu Mwenye Nguvu, Baba wa Milele, Mfalme wa Amani.
Mamlaka ya enzi yake yatakuzwa daima, Na kutakuwa na amani isiyo na mwisho, Katika kiti cha enzi cha Daudi na ufalme wake; Kuuthibitisha na kuutegemeza Kwa hukumu na kwa haki, Tangu sasa na hata milele. Wivu wa BWANA wa majeshi ndio utakaotenda hayo.
Haya ndiyo mtakayoyatenda; kila mtu na aseme ukweli na jirani yake; katika malango yenu toeni hukumu za kweli na ziletazo amani;
katika neno la kweli, katika nguvu ya Mungu; kwa silaha za haki za mkono wa kulia na za mkono wa kushoto;
Hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, ili afanye kafara ya suluhu kwa dhambi za watu wake.
Basi kwa kuwa Kristo aliteswa katika mwili wake, ninyi nanyi jivikeni silaha ya nia ile ile; kwa maana yeye aliyeteswa katika mwili ameachana na dhambi.
Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kututakasa na udhalimu wote.
na katikati ya vile vinara nikaona mtu mfano wa Mwanadamu, amevaa vazi lililofika miguuni, na kufungwa mshipi wa dhahabu kifuani
Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu.