Nanyi kweli mlinikusudia mabaya, bali Mungu aliyakusudia kuwa mema, ili itokee kuokoa taifa kubwa, kama ilivyo leo.
Isaya 10:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Lakini hivyo sivyo akusudiavyo mwenyewe, wala sivyo moyo wake uwazavyo; maana katika moyo wake akusudia kuharibu, na kukatilia mbali mataifa, wala si mataifa machache. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini Ashuru hakudhamiria hivyo, yeye alikuwa na nia nyingine; alikusudia kuharibu kabisa, kuangamiza mataifa mengi iwezekanavyo. Biblia Habari Njema - BHND Lakini Ashuru hakudhamiria hivyo, yeye alikuwa na nia nyingine; alikusudia kuharibu kabisa, kuangamiza mataifa mengi iwezekanavyo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini Ashuru hakudhamiria hivyo, yeye alikuwa na nia nyingine; alikusudia kuharibu kabisa, kuangamiza mataifa mengi iwezekanavyo. Neno: Bibilia Takatifu Lakini hili silo analokusudia, hili silo alilo nalo akilini; kusudi lake ni kuangamiza, kuyakomesha mataifa mengi. Neno: Maandiko Matakatifu Lakini hili silo analokusudia, hili silo alilo nalo akilini; kusudi lake ni kuangamiza, kuyakomesha mataifa mengi. BIBLIA KISWAHILI Lakini hivyo sivyo akusudiavyo mwenyewe, wala sivyo moyo wake uwazavyo; maana katika moyo wake akusudia kuharibu, na kukatilia mbali mataifa, wala si mataifa machache. |
Nanyi kweli mlinikusudia mabaya, bali Mungu aliyakusudia kuwa mema, ili itokee kuokoa taifa kubwa, kama ilivyo leo.
Tazama, nchi ya Wakaldayo; watu hao hawako tena; Mwashuri ameiweka tayari kwa hayawani wa jangwani; wamesimamisha ngome zao za vita, wameyaharibu majumba yake ya enzi, akaufanya kuwa uharibifu.
na kuwatupa miungu yao motoni; kwa maana hao hawakuwa miungu, bali kazi ya mikono ya wanadamu; walikuwa miti na mawe, ndiyo sababu wakawaharibu.
Nimempa nchi ya Misri kuwa malipo ya kazi aliyofanya, kwa sababu walifanya kazi kwa ajili yangu; asema Bwana MUNGU.
Atakapokwisha kuchukua lile jeshi, moyo wake utatukuzwa; naye atawaangusha makumi ya maelfu; lakini hataongezewa nguvu.
mtu huyu alipotolewa kwa shauri la Mungu lililokusudiwa, na kwa kujua kwake tangu zamani, ninyi mkamsulubisha kwa mikono ya watu wabaya, mkamwua;
ambaye Mungu alimfufua, akiufungua uchungu wa mauti, kwa sababu haikuwezekana ashikwe nao.