Wana wa Benyamini nao walikuwa wakikaa Geba, na Mikmashi, na Aiya, na Betheli na vijiji vyake;
Isaya 10:28 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Amefika Ayathi; amepita kati ya Migroni; ameweka mizigo yake huko Mikmashi; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema amefika mjini Ayathi. Amepitia huko Migroni, mizigo yake ameiacha Mikmashi. Biblia Habari Njema - BHND amefika mjini Ayathi. Amepitia huko Migroni, mizigo yake ameiacha Mikmashi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza amefika mjini Ayathi. Amepitia huko Migroni, mizigo yake ameiacha Mikmashi. Neno: Bibilia Takatifu Wanaingia Ayathi, wanapita katikati ya Migroni, wanahifadhi mahitaji huko Mikmashi. Neno: Maandiko Matakatifu Wanaingia Ayathi, wanapita katikati ya Migroni, wanahifadhi mahitaji huko Mikmashi. BIBLIA KISWAHILI Amefika Ayathi; amepita kati ya Migroni; ameweka mizigo yake huko Mikmashi; |
Wana wa Benyamini nao walikuwa wakikaa Geba, na Mikmashi, na Aiya, na Betheli na vijiji vyake;
naye atapita, atapita kwa kasi na kuingia Yuda; atafurika na kupita katikati, atafika hadi shingoni; na kule kuyanyosha mabawa yake kutaujaza upana wa nchi yako, Ee Imanueli.
Kwa maana majeraha yake hayaponyeki; Maana msiba umeijia hata Yuda, Unalifikia lango la watu wangu, Naam, hata Yerusalemu.
Kisha Yoshua akatuma watu kutoka Yeriko mpaka mji wa Ai, ulio karibu na Beth-aveni, upande wa mashariki wa Betheli, akawaambia, akisema, Pandeni juu mkaipeleleze nchi, basi wakapanda juu wakaupeleleza Ai.
Basi wakageuka wakaenda zao, lakini watoto wadogo na wanyama wao wa kufugwa, na vyombo vyao, wakawatanguliza mbele yao.
Naye Sauli alijichagulia watu elfu tatu wa Israeli; ambao katika hao, elfu mbili walikuwa pamoja na Sauli katika Mikmashi, na katika mlima wa Betheli na elfu moja pamoja na Yonathani katika Gibea ya Benyamini; nao wale watu waliosalia akawaruhusu waende kila mtu hemani kwake.
Nao Wafilisti wakakusanyika ili wapigane na Waisraeli, magari elfu thelathini, na wapanda farasi elfu sita, na watu kama mchanga ulio ufuoni mwa bahari kwa wingi wao; wakapanda juu, wakapiga kambi yao katika Mikmashi, upande wa mashariki wa Beth-aveni.
Naye Sauli alikuwa akikaa katika Viunga vya Gibea, chini ya mkomamanga uliokuwa kwenye uwanja huko Migroni; na hao watu waliokuwa pamoja naye walikuwa watu mia sita;
Nao wakawapiga watu miongoni mwa Wafilisti siku ile kutoka Mikmashi mpaka Ayaloni; na hao watu walikuwa wamepungukiwa sana na nguvu.
Hicho kilima kimoja kimesimama upande wa kaskazini, mbele ya Mikmashi, na hicho cha pili upande wa kusini, mbele ya Geba.
Basi Daudi akaviacha vile vyombo vyake katika mkono wa mlinda vyombo, akalikimbilia jeshi, akafika, akawasalimu ndugu zake.