Abramu akapita katikati ya nchi mpaka mahali patakatifu pa Shekemu; mpaka mwaloni wa More. Na Wakanaani siku zile walikaa katika nchi hiyo.
Isaya 1:30 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Maana mtakuwa kama mwaloni ambao majani yake yakauka, na kama bustani isiyo na maji. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mtakuwa kama mwaloni unaonyauka majani; kama shamba lisilo na maji. Biblia Habari Njema - BHND Mtakuwa kama mwaloni unaonyauka majani; kama shamba lisilo na maji. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mtakuwa kama mwaloni unaonyauka majani; kama shamba lisilo na maji. Neno: Bibilia Takatifu Mtakuwa kama mwaloni ulio na majani yanayonyauka, kama bustani isiyokuwa na maji. Neno: Maandiko Matakatifu Mtakuwa kama mwaloni wenye majani yanayonyauka, kama bustani isiyokuwa na maji. BIBLIA KISWAHILI Maana mtakuwa kama mwaloni ambao majani yake yakauka, na kama bustani isiyo na maji. |
Abramu akapita katikati ya nchi mpaka mahali patakatifu pa Shekemu; mpaka mwaloni wa More. Na Wakanaani siku zile walikaa katika nchi hiyo.
nami nitaliharibu; wala halitapogolewa wala kulimwa, bali litamea mbigili na miiba; nami nitayaamuru mawingu yasinyeshe mvua juu yake.
Naye BWANA atakuongoza daima, ataishibisha nafsi yako mahali pasipokuwa na maji, na kuitia nguvu mifupa yako; nawe utakuwa kama bustani iliyotiwa maji, na kama chemchemi ambayo maji yake hayapungui.
Wewe wamlaki yeye afurahiaye yaliyo haki na kuyatenda, watu wale wakukumbukao katika njia zako; tazama, ulikuwa na hasira, nasi tulitenda dhambi; tumekuwa katika dhambi kwa muda mrefu, nasi Je! Tutaokolewa?
Kwa maana sisi sote tumekuwa kama mtu aliye mchafu, na matendo yetu yote ya haki yamekuwa kama nguo iliyotiwa unajisi; sisi sote twanyauka kama jani, na maovu yetu yatuondoa, kama upepo uondoavyo.
Nao watakuja, na kuimba katika mlima Sayuni, wataukimbilia wema wa BWANA, nafaka, na divai, na mafuta, na wachanga wa kondoo na wa ng'ombe; na roho zao zitakuwa kama bustani iliyotiwa maji; wala hawatahuzunika tena kabisa.
Na miti yote ya mashamba itajua ya kuwa mimi, BWANA, nimeushusha chini mti mrefu, na kuuinua mti mfupi, na kuukausha mti mbichi, na kuusitawisha mti mkavu; mimi, BWANA, nimenena, nami nimelitenda jambo hili.
Akaona mtini mmoja kando ya njia, akauendea, asione kitu juu yake ila majani tu; akauambia, Yasipatikane matunda kwako tangu leo hata milele. Mtini ukanyauka mara.