Na hao waliokombolewa na BWANA watarudi, watafika Sayuni wakiimba; na furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao; nao watapata kicheko na furaha, huzuni na kuugua zitatoweka.
Isaya 1:27 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Sayuni itakombolewa kwa hukumu, na waongofu wake kwa haki. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mji Siyoni utakombolewa kwa haki, uadilifu utawaokoa watakaotubu humo. Biblia Habari Njema - BHND Mji Siyoni utakombolewa kwa haki, uadilifu utawaokoa watakaotubu humo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mji Siyoni utakombolewa kwa haki, uadilifu utawaokoa watakaotubu humo. Neno: Bibilia Takatifu Sayuni itakombolewa kwa haki, wale walio ndani yake waliotubu, kwa uaminifu. Neno: Maandiko Matakatifu Sayuni itakombolewa kwa haki, wale waliomo ndani yake waliotubu kwa uaminifu. BIBLIA KISWAHILI Sayuni itakombolewa kwa hukumu, na waongofu wake kwa haki. |
Na hao waliokombolewa na BWANA watarudi, watafika Sayuni wakiimba; na furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao; nao watapata kicheko na furaha, huzuni na kuugua zitatoweka.
Hapo hapatakuwa na simba, wala mnyama mkali hatapanda juu yake; hawataonekana hapo; bali waliokombolewa watakwenda katika njia hiyo.
bali BWANA wa majeshi ametukuzwa katika hukumu, na Mungu aliye Mtakatifu ametakaswa katika haki.
Nisikilizeni mimi, enyi watu wangu; nisikieni, taifa langu; maana sheria itatoka kwangu, na kutoa haki yangu iwe nuru ya mataifa.
Utathibitika katika haki; utakuwa mbali na kuonewa, kwa maana hutaogopa; na mbali na hofu, kwa maana haitakukaribia.
Nao watawaita, Watu watakatifu, Waliokombolewa na BWANA; Nawe utaitwa, Aliyetafutwa, Mji usioachwa.
Nami nitakuposa uwe wangu wa milele; naam, nitakuposa kwa haki, na kwa hukumu, na kwa ufadhili, na kwa rehema.
Enyi watu wangu, kumbukeni sasa alivyouliza Balaki, mfalme wa Moabu, na alivyojibu Balaamu, mwana wa Beori; kumbukeni yaliyotukia toka Shitimu hadi Gilgali, mpate kuyajua matendo ya haki ya BWANA.
Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanywa kwetu hekima itokayo kwa Mungu, na haki, na utakatifu, na ukombozi;
Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye.
ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wake mwenyewe walio na bidii katika matendo mema.