Hapo ndipo waliposema, Njooni na tufanye mashauri juu ya Yeremia; maana sheria haitampotea kuhani, wala shauri halitampotea mwenye hekima, wala neno halitampotea nabii. Njooni, na tumpige kwa ndimi zetu, wala tusiyaangalie maneno yake yoyote.
Hosea 4:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Lakini asishindane mtu, wala mtu asikemee; maana watu wako ni kama wao washindanao na kuhani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Lakini watu wasilaumiwe, wasishutumiwe; maana mimi nakushutumu wewe kuhani. Biblia Habari Njema - BHND “Lakini watu wasilaumiwe, wasishutumiwe; maana mimi nakushutumu wewe kuhani. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Lakini watu wasilaumiwe, wasishutumiwe; maana mimi nakushutumu wewe kuhani. Neno: Bibilia Takatifu “Lakini mtu yeyote na asilete shtaka, mtu yeyote na asimlaumu mwenzake, kwa maana watu wako ni kama wale waletao mashtaka dhidi ya kuhani. Neno: Maandiko Matakatifu “Lakini mtu awaye yote na asilete shtaka, mtu yeyote na asimlaumu mwenzake, kwa maana watu wako ni kama wale waletao mashtaka dhidi ya kuhani. BIBLIA KISWAHILI Lakini asishindane mtu, wala mtu asikemee; maana watu wako ni kama wao washindanao na kuhani. |
Hapo ndipo waliposema, Njooni na tufanye mashauri juu ya Yeremia; maana sheria haitampotea kuhani, wala shauri halitampotea mwenye hekima, wala neno halitampotea nabii. Njooni, na tumpige kwa ndimi zetu, wala tusiyaangalie maneno yake yoyote.
nami nitaufanya ulimi wako ugandamane na kaakaa lako, hata utakuwa bubu, wala hutakuwa mwonyaji kwao; kwa kuwa wao ni nyumba yenye kuasi.
Kwa ajili ya hayo mwenye busara atanyamaza kimya wakati kama huo; kwa kuwa ni wakati mbaya.
Na mjomba wa mtu atakapomwinua, yaani, yeye amchomaye moto, ili atoe mifupa yake nyumbani, naye atakapomwambia yeye aliye katika pande za ndani za nyumba, Je! Yuko mtu yeyote pamoja nawe? Naye atakaposema, La, hapana; ndipo atasema, Nyamaza kimya; maana hatuna ruhusa kulitaja jina la BWANA.
Na mtu afanyaye kwa kujikinai, kwa kutomsikiza kuhani asimamaye hapo kwa kumtumikia BWANA, Mungu wako, au mwamuzi, na afe mtu huyo; nawe utauondoa uovu katika Israeli.