Katika siku za Peka mfalme wa Israeli akaja Tiglath-pileseri mfalme wa Ashuru, akatwaa Iyoni, na Abel-beth-maaka, na Yanoa, na Kedeshi, na Hazori, na Gileadi, na Galilaya, nchi yote ya Naftali; akawahamisha hao watu mpaka Ashuru.
Hosea 1:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Tena itakuwa siku ile, nitauvunja upinde wa Israeli katika bonde la Yezreeli. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Siku hiyo, nitazivunja nguvu za kijeshi za Israeli huko bondeni Yezreeli.” Biblia Habari Njema - BHND Siku hiyo, nitazivunja nguvu za kijeshi za Israeli huko bondeni Yezreeli.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Siku hiyo, nitazivunja nguvu za kijeshi za Israeli huko bondeni Yezreeli.” Neno: Bibilia Takatifu Katika siku ile nitavunja upinde wa Israeli katika Bonde la Yezreeli.” Neno: Maandiko Matakatifu Katika siku ile nitavunja upinde wa Israeli katika Bonde la Yezreeli.” BIBLIA KISWAHILI Tena itakuwa siku ile, nitauvunja upinde wa Israeli katika bonde la Yezreeli. |
Katika siku za Peka mfalme wa Israeli akaja Tiglath-pileseri mfalme wa Ashuru, akatwaa Iyoni, na Abel-beth-maaka, na Yanoa, na Kedeshi, na Hazori, na Gileadi, na Galilaya, nchi yote ya Naftali; akawahamisha hao watu mpaka Ashuru.
Kwa maana mwenye kuangamiza amefika kwake; Naam, amefika Babeli; Na mashujaa wake wametwaliwa; Pinde zao zimevunjika kabisa; Maana BWANA ni Mungu wa kisasi; Hakika yake yeye atalipa.
nami nitaupiga upinde wako, utoke katika mkono wako wa kushoto, na mishale yako nitaiangusha, itoke katika mkono wako wa kulia.
Nami siku hiyo nitafanya agano na wanyama wa mashamba kwa ajili yao, tena na ndege wa angani, tena na wadudu wa nchi; nami nitavivunja upinde na upanga na silaha vitoke katika nchi, nami nitawalalisha salama salimini.
Wana wa Yusufu wakasema, Hiyo nchi ya vilima haitutoshi sisi; lakini Wakanaani wote wakaao katika nchi ya bondeni wana magari ya chuma, hao walio katika Beth-sheani na miji yake, na hao walio katika bonde la Yezreeli pia.
Wakati huo Wamidiani na Waamaleki, na hao wana wa mashariki walikutana pamoja; wakavuka na kupanga hema zao katika bonde la Yezreeli.