nawe utavitia hivi vyote katika mikono ya Haruni, na katika mikono ya wanawe; nawe utavitikisatikisa viwe sadaka ya kutikiswa mbele za BWANA.
Hesabu 8:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kisha baadaye Walawi wataingia ndani, ili wahudumu katika hema ya kukutania; nawe utawatakasa, na kuwasongeza wawe sadaka ya kutikiswa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Baada ya kuwatakasa Walawi na kuwatoa kama sadaka ya kutikiswa wataingia ili kuhudumu katika hema la mkutano. Biblia Habari Njema - BHND Baada ya kuwatakasa Walawi na kuwatoa kama sadaka ya kutikiswa wataingia ili kuhudumu katika hema la mkutano. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Baada ya kuwatakasa Walawi na kuwatoa kama sadaka ya kutikiswa wataingia ili kuhudumu katika hema la mkutano. Neno: Bibilia Takatifu “Utakapokuwa umekwisha kuwatakasa Walawi na kuwatoa wawe sadaka ya kuinuliwa, watakuja kufanya kazi yao katika Hema la Kukutania. Neno: Maandiko Matakatifu “Utakapokuwa umekwisha kuwatakasa Walawi na kuwatoa kama sadaka ya kuinuliwa, watakuja kufanya kazi yao katika Hema la Kukutania. BIBLIA KISWAHILI Kisha baadaye Walawi wataingia ndani, ili wahudumu katika hema ya kukutania; nawe utawatakasa, na kuwasongeza wawe sadaka ya kutikiswa. |
nawe utavitia hivi vyote katika mikono ya Haruni, na katika mikono ya wanawe; nawe utavitikisatikisa viwe sadaka ya kutikiswa mbele za BWANA.
Mimi, tazama, nimewateua Walawi na kuwatoa kati ya wana wa Israeli badala ya kila mzaliwa wa kwanza wote wafunguao tumbo katika wana wa Israeli; na hao Walawi watakuwa wangu;
naye Haruni atawasongeza Walawi mbele za BWANA wawe sadaka ya kutikiswa, kwa ajili ya wana wa Israeli, ili wawe watumishi wa BWANA.
Kisha utawaweka Walawi mbele ya Haruni, na mbele ya wanawe na kuwasongeza kwa BWANA wawe sadaka ya kutikiswa.
Kwa kuwa nimepewa kabisa mimi watu hawa kutoka katika wana wa Israeli; badala ya wote wafunguao mimba, maana, wazaliwa wa kwanza wa wana wa Israeli wote, nimewatwaa wawe wangu.