Hesabu 6:27 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ndivyo watakavyoweka jina langu juu ya wana wa Israeli; nami nitawabariki. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Ndivyo watakavyotamka jina langu juu ya Waisraeli, nami nitawabariki.” Biblia Habari Njema - BHND “Ndivyo watakavyotamka jina langu juu ya Waisraeli, nami nitawabariki.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Ndivyo watakavyotamka jina langu juu ya Waisraeli, nami nitawabariki.” Neno: Bibilia Takatifu “Hivyo wataliweka Jina langu juu ya Waisraeli, nami nitawabariki.” Neno: Maandiko Matakatifu “Hivyo wataliweka Jina langu juu ya Waisraeli, nami nitawabariki.” BIBLIA KISWAHILI Ndivyo watakavyoweka jina langu juu ya wana wa Israeli; nami nitawabariki. |
Yakobo akamwuliza, akasema, Niambie, tafadhali, jina lako? Akasema, Kwa nini waniuliza jina langu? Akambariki huko.
Tena ni taifa lipi duniani lililo kama watu wako, kama Israeli, ambalo Mungu alikwenda kuwakomboa kwa ajili yake, wawe watu wake mwenyewe, akajifanyie jina, na kutenda mambo makuu kwa ajili yenu, na mambo ya kuogofya kwa ajili ya nchi yako, mbele ya watu wako, uliowakomboa kutoka Misri wawe wako, kutoka katika mataifa na miungu yao.
Huyo Yabesi akamlingana Mungu wa Israeli, akisema, Lau kwamba ungenibariki kweli kweli, na kuipanua mipaka yangu, na mkono wako ukawa pamoja nami, nawe ungenilinda nisipatwe na maovu wala madhara! Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba.
ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekeza, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.
nami nilimtokea Abrahamu, na Isaka, na Yakobo, kama Mungu Mwenyezi, bali kwa jina langu YEHOVA sikujulikana kwao.
Kila mmoja aliyeitwa kwa jina langu, niliyemwumba kwa ajili ya utukufu wangu; mimi nimemwumba, naam, mimi nimemfanya.
Kwa nini wewe umekuwa kama mtu aliyeshtuka, kama shujaa asiyeweza kuokoa? Lakini wewe, BWANA, u katikati yetu, nasi tunaitwa kwa jina lako; usituache.
Basi, nendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo;
Na mataifa yote ya duniani watakuona umeitwa kwa jina la BWANA, nao watakuwa na hofu kwako.