Tena katika Yuda mkono wa Mungu ulikuwa ukiwapa moyo mmoja, waitimize amri ya mfalme na wakuu kwa neno la BWANA.
Hesabu 36:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Basi hao binti za Selofehadi wakafanya kama BWANA alivyomwagiza Musa; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Binti za Selofehadi walifanya kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose. Biblia Habari Njema - BHND Binti za Selofehadi walifanya kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Binti za Selofehadi walifanya kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose. Neno: Bibilia Takatifu Kwa hiyo binti za Selofehadi wakafanya kama Mwenyezi Mungu alivyomwamuru Musa. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa hiyo binti za Selofehadi wakafanya kama bwana alivyomwamuru Musa. BIBLIA KISWAHILI Basi hao binti za Selofehadi wakafanya kama BWANA alivyomwagiza Musa; |
Tena katika Yuda mkono wa Mungu ulikuwa ukiwapa moyo mmoja, waitimize amri ya mfalme na wakuu kwa neno la BWANA.
Ndivyo walivyofanya wana wa Israeli wote; kama BWANA alivyowaagiza Musa na Haruni, ndivyo walivyofanya.
Musa akanena na wana wa Israeli, nao wakamtoa huyo aliyeapiza nje ya kambi, wakamwua kwa kumpiga kwa mawe. Wana wa Israeli wakafanya kama BWANA alivyomwagiza Musa.
Ndivyo walivyofanya wana wa Israeli; kama yote BWANA aliyomwagiza Musa, ndivyo walivyofanya.
kwa kuwa Mala, na Tirza, na Hogla, na Milka, na Nuhu, binti za Selofehadi waliolewa na wanaume, wana wa ndugu za baba yao.
Hivyo hapatakuwa na urithi wowote utakaotoka kabila hili kwenda kabila hili; kwa kuwa makabila ya wana wa Israeli yatashikamana kila mmoja na urithi wake mwenyewe.
na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
Nao wakaja mbele ya kuhani Eleazari, kuhani, na mbele ya Yoshua, mwana wa Nuni, na mbele ya viongozi, wakasema, BWANA alimwamuru Musa kutupa sisi urithi kati ya ndugu zetu; basi kwa kuifuata hiyo amri ya BWANA akawapa urithi kati ya ndugu za baba yao.