Tutavuka, tukiwa tumevaa silaha zetu, mbele za BWANA, kuingia nchi ya Kanaani, nayo milki ya urithi wetu itakuwa ng'ambo ya pili ya Yordani.
Hesabu 34:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC hayo makabila mawili na nusu ya kabila wamekwisha pata urithi wao huko ng'ambo ya pili ya Yordani, hapo Yeriko, upande wa mashariki, kuelekea maawio ya jua. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Makabila hayo mawili na nusu yamepata urithi wao ngambo ya mto Yordani upande wa mashariki, mkabala wa Yeriko, mawioni.” Biblia Habari Njema - BHND Makabila hayo mawili na nusu yamepata urithi wao ngambo ya mto Yordani upande wa mashariki, mkabala wa Yeriko, mawioni.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Makabila hayo mawili na nusu yamepata urithi wao ng'ambo ya mto Yordani upande wa mashariki, mkabala wa Yeriko, mawioni.” Neno: Bibilia Takatifu Haya makabila mawili na nusu wamekwishapokea urithi wao upande wa mashariki wa Yordani ng’ambo ya Yeriko, kuelekea mawio ya jua.” Neno: Maandiko Matakatifu Haya makabila mawili na nusu wamekwishapokea urithi wao upande wa mashariki wa Yordani ng’ambo ya Yeriko, kuelekea mawio ya jua.” BIBLIA KISWAHILI hayo makabila mawili na nusu ya kabila wamekwisha pata urithi wao huko ng'ambo ya pili ya Yordani, hapo Yeriko, upande wa mashariki, kuelekea mawio ya jua. |
Tutavuka, tukiwa tumevaa silaha zetu, mbele za BWANA, kuingia nchi ya Kanaani, nayo milki ya urithi wetu itakuwa ng'ambo ya pili ya Yordani.
Basi Musa akawapa wao, maana, wana wa Gadi, na wana wa Reubeni, na hiyo nusu ya kabila la Manase, mwana wa Yusufu, ufalme wa Sihoni mfalme wa Waamori, na ufalme wa Ogu mfalme wa Bashani, hiyo nchi, kama miji yao ilivyokuwa, pamoja na mipaka yake, maana, miji ya hiyo nchi iliyozunguka kotekote.
kwa kuwa kabila la wana wa Reubeni kwa nyumba za baba zao, na kabila la wana wa Gadi kwa nyumba za baba zao, wamekwisha pata, na hiyo nusu ya kabila la Manase wamekwisha pata urithi wao;
ili kufukuza mbele yako mataifa, walio wakubwa, wenye nguvu kukupita wewe, ili kukuingiza, na kukupa nchi yao iwe urithi, kama ilivyo leo.