Siku ile BWANA akafanya agano na Abramu, akasema, Uzao wako nimewapa nchi hii, kutoka mto wa Misri mpaka huo mto mkubwa, mto Frati,
Hesabu 34:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kisha Musa akawaagiza wana wa Israeli, akisema, Hii ndiyo nchi mtakayoirithi kwa kupiga kura, ambayo BWANA ameagiza wapewe watu wa yale makabila tisa, na nusu ya kabila; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, Mose akawaambia Waisraeli, “Hii ndiyo nchi mtakayoirithi kwa kupiga kura, nchi ambayo Mwenyezi-Mungu ameagiza yapewe makabila tisa na nusu. Biblia Habari Njema - BHND Basi, Mose akawaambia Waisraeli, “Hii ndiyo nchi mtakayoirithi kwa kupiga kura, nchi ambayo Mwenyezi-Mungu ameagiza yapewe makabila tisa na nusu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, Mose akawaambia Waisraeli, “Hii ndiyo nchi mtakayoirithi kwa kupiga kura, nchi ambayo Mwenyezi-Mungu ameagiza yapewe makabila tisa na nusu. Neno: Bibilia Takatifu Musa akawaamuru Waisraeli: “Gawanyeni nchi hii kwa kura kama urithi. Mwenyezi Mungu ameagiza kwamba itolewe kwa yale makabila tisa na nusu, Neno: Maandiko Matakatifu Musa akawaamuru Waisraeli: “Gawanyeni nchi hii kwa kura kama urithi. bwana ameagiza kwamba itolewe kwa yale makabila tisa na nusu, BIBLIA KISWAHILI Kisha Musa akawaagiza wana wa Israeli, akisema, Hii ndiyo nchi mtakayoirithi kwa kupiga kura, ambayo BWANA ameagiza wapewe watu wa yale makabila tisa, na nusu ya kabila; |
Siku ile BWANA akafanya agano na Abramu, akasema, Uzao wako nimewapa nchi hii, kutoka mto wa Misri mpaka huo mto mkubwa, mto Frati,
Tena, mtakapoigawanya nchi kwa kura iwe urithi, mtamtolea BWANA toleo, sehemu takatifu ya nchi, urefu wake utakuwa urefu wa mianzi elfu ishirini na tano, na upana wake elfu kumi; itakuwa takatifu ndani ya mipaka yake yote pande zote.
Lakini nchi itagawanywa kwa kura; kwa majina ya makabila ya baba zao, ndivyo watakavyopata urithi.
kisha mpaka utateremkia Yordani, na kutokea kwake kutakuwa hapo katika Bahari ya Chumvi; hii ndiyo nchi yenu kama mipaka yake ilivyo kuizunguka pande zote.
Kila mahali mtakapokanyaga kwa nyayo za miguu yenu patakuwa penu; tokea hilo jangwa, na Lebanoni, na tokea mto wa Frati, mpaka bahari ya magharibi, itakuwa ndiyo mipaka yenu.
Basi sasa gawanya nchi hii, iwe urithi wa hizi kabila tisa, na nusu ya kabila la Manase.