Siku ile BWANA akafanya agano na Abramu, akasema, Uzao wako nimewapa nchi hii, kutoka mto wa Misri mpaka huo mto mkubwa, mto Frati,
Hesabu 34:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, Biblia Habari Njema - BHND Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, Neno: Bibilia Takatifu Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, Neno: Maandiko Matakatifu bwana akamwambia Musa, BIBLIA KISWAHILI Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, |
Siku ile BWANA akafanya agano na Abramu, akasema, Uzao wako nimewapa nchi hii, kutoka mto wa Misri mpaka huo mto mkubwa, mto Frati,
Wakamwambia, Sisi watumwa wako tu ndugu kumi na wawili, wana wa mtu mmoja katika nchi ya Kanaani; na mdogo wetu yuko pamoja na baba yetu leo, na mmoja hayuko.
Bwana MUNGU asema hivi; Huu ndio mpaka ambao mtaigawanya nchi iwe urithi sawasawa na makabila kumi na mawili ya Israeli; kwa Yusufu, mafungu mawili.
Akasimama na kuitikisa dunia; Akatazama, mataifa yakatetemeka; Na milima ya zamani ikatawanyika; Vilima vya kale vikainama; Miendo yake ilikuwa kama siku za kale.
Kisha Musa akawaagiza wana wa Israeli, akisema, Hii ndiyo nchi mtakayoirithi kwa kupiga kura, ambayo BWANA ameagiza wapewe watu wa yale makabila tisa, na nusu ya kabila;
Waagize wana wa Israeli, uwaambie, Mtakapoingia nchi ya Kanaani, (hii ndiyo nchi itakayowaangukia kuwa urithi, maana, hiyo nchi ya Kanaani kama mipaka yake ilivyo,)