Hesabu 32:24 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Basi, jengeni miji kwa ajili ya watoto wenu, na mazizi kwa ajili ya kondoo zenu; mkayafanye hayo mliotamka kwa vinywa vyenu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wajengeeni watoto wenu miji na kondoo wenu mazizi; lakini fanyeni kama mlivyoahidi.” Biblia Habari Njema - BHND Wajengeeni watoto wenu miji na kondoo wenu mazizi; lakini fanyeni kama mlivyoahidi.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wajengeeni watoto wenu miji na kondoo wenu mazizi; lakini fanyeni kama mlivyoahidi.” Neno: Bibilia Takatifu Jengeni miji kwa ajili ya wanawake na watoto wenu, na mazizi kwa ajili ya mbuzi na kondoo wenu, lakini fanyeni yale mliyoahidi.” Neno: Maandiko Matakatifu Jengeni miji kwa ajili ya wanawake na watoto wenu, na mazizi kwa ajili ya mbuzi na kondoo zenu, lakini fanyeni yale mliyoahidi.” BIBLIA KISWAHILI Basi, jengeni miji kwa ajili ya watoto wenu, na mazizi kwa ajili ya kondoo zenu; mkayafanye hayo mliyotamka kwa vinywa vyenu. |
Mtu atakapomwekea BWANA nadhiri, au, atakapoapa kiapo ili kufunga nafsi yake kwa ahadi, asilitangue neno lake; atafanya sawasawa na hayo yote yamtokayo kinywani mwake.
Basi wakamwendea karibu, na kusema, Sisi tutafanya mazizi hapa kwa ajili ya mifugo yetu, na kujenga miji kwa ajili ya watoto wetu;
Ndipo wana wa Gadi na wana wa Reubeni wakanena na Musa, na kumwambia, Sisi watumishi wako tutafanya kama wewe bwana wangu utuagizavyo.