Hesabu 32:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na siku ile hasira za BWANA ziliwaka, naye akaapa, akisema, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenyezi-Mungu aliwaka hasira siku hiyo, akaapa akisema, Biblia Habari Njema - BHND Mwenyezi-Mungu aliwaka hasira siku hiyo, akaapa akisema, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenyezi-Mungu aliwaka hasira siku hiyo, akaapa akisema, Neno: Bibilia Takatifu Siku ile hasira ya Mwenyezi Mungu iliwaka naye akaapa kiapo hiki: Neno: Maandiko Matakatifu Siku ile hasira ya bwana iliwaka naye akaapa kiapo hiki: BIBLIA KISWAHILI Na siku ile hasira za BWANA ziliwaka, naye akaapa, akisema, |
Tena niliwainulia mkono wangu jangwani, ya kwamba sitawaingiza katika nchi ile niliyokuwa nimewapa, itiririkayo maziwa na asali, ambayo ni utukufu wa nchi zote;
BWANA akamwuliza Musa, Je! Watu hawa watanidharau hadi lini? Wasiniamini hadi lini? Nijapokuwa nimefanya ishara hizo zote kati yao.
lakini hakika yangu, kama niishivyo, tena kama dunia hii nzima itakavyojawa na utukufu wa BWANA;
hakika yangu hawataiona hiyo nchi niliyowaapia baba zao, wala katika hao wote walionidharau hapana atakayeiona;
mizoga yenu itaanguka katika jangwa hili, na wote waliohesabiwa miongoni mwenu, kama jumla ya hesabu yenu, tangu waliopata umri wa miaka ishirini na zaidi, hao walioninung'unikia,