Wakatwaa na mali yao zote, watoto wao wote, na wake zao wakateka na hata wakapora vyote vilivyokuwemo nyumbani.
Hesabu 31:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Wana wa Israeli wakawachukua mateka wanawake wa Midiani na watoto wao; na ng'ombe zao wote, na kondoo zao wote, na mali zao zote, wakachukua nyara. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Waisraeli waliteka nyara: Ng'ombe, kondoo na mali yao yote. Biblia Habari Njema - BHND Waisraeli waliteka nyara: Ng'ombe, kondoo na mali yao yote. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Waisraeli waliteka nyara: ng'ombe, kondoo na mali yao yote. Neno: Bibilia Takatifu Waisraeli waliwateka wanawake wa Midiani pamoja na watoto wao, na wakachukua makundi ya ng’ombe, kondoo na mali yao kama nyara. Neno: Maandiko Matakatifu Waisraeli waliwateka wanawake wa Kimidiani pamoja na watoto wao na walichukua makundi ya ng’ombe, kondoo na mali zao kama nyara. BIBLIA KISWAHILI Wana wa Israeli wakawachukua mateka wanawake wa Midiani na watoto wao; na ng'ombe wao wote, na kondoo wao wote, na mali zao zote, wakachukua nyara. |
Wakatwaa na mali yao zote, watoto wao wote, na wake zao wakateka na hata wakapora vyote vilivyokuwemo nyumbani.
Kwa hiyo BWANA, Mungu wake, akamtia mkononi mwa mfalme wa Shamu; wakampiga, wakachukua wa watu wake wafungwa wengi sana, wakawaleta Dameski. Tena akatiwa mkononi mwa mfalme wa Israeli, aliyempiga mapigo makuu.
Na miji yao yote, kila mahali walipokuwa wakikaa, na kambi yao yote wakayateketeza kwa moto.
Nao wafalme wa Midiani wakawaua pamoja na watu wengine waliouawa; Evi, na Rekemu, na Suri, na Huri, na Reba, hao wafalme watano wa Midiani; Balaamu mwana wa Beori naye wakamwua kwa upanga.
lakini wanawake na watoto, na wanyama wa miji, na vilivyo mjini vyote, navyo ni nyara zake zote, uvitwae viwe mateka kwako; nawe utakula nyara za adui zako alizokupa BWANA, Mungu wako.