Na alaaniwe mtu afanyaye kazi ya BWANA kwa ulegevu; na alaaniwe auzuiaye upanga wake usimwage damu.
Hesabu 31:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Musa akawauliza, Je! Mmewaponya wanawake wote hai? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mose akawauliza, “Kwa nini mmewaacha wanawake hawa wote hai? Biblia Habari Njema - BHND Mose akawauliza, “Kwa nini mmewaacha wanawake hawa wote hai? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mose akawauliza, “Kwa nini mmewaacha wanawake hawa wote hai? Neno: Bibilia Takatifu Musa akawauliza, “Je, mmewaacha wanawake wote hai? Neno: Maandiko Matakatifu Musa akawauliza, “Je, mmewaacha wanawake wote hai?” BIBLIA KISWAHILI Musa akawauliza, Je! Mmewaponya wanawake wote hai? |
Na alaaniwe mtu afanyaye kazi ya BWANA kwa ulegevu; na alaaniwe auzuiaye upanga wake usimwage damu.
Waueni kabisa, wazee, na viijana, na wasichana, na watoto wachanga, na wanawake; lakini msimkaribie mtu yeyote mwenye hiyo alama; tena anzeni katika patakatifu pangu. Basi, wakaanza kwa wazee waliokuwa mbele ya nyumba.
Musa akawakasirikia majemadari wa jeshi, na hao makamanda wa maelfu, na makamanda wa mamia, hao waliorudi kutoka kupigana vita.
Tukatwaa miji yake yote wakati huo, tukaharibu kabisa kila mji uliokuwa na wanaume, wanawake na watoto; tusimbakize hata mmoja;
na BWANA, Mungu wako, autiapo mkononi mwako, mpige kila mume aliyemo kwa makali ya upanga;
lakini wanawake na watoto, na wanyama wa miji, na vilivyo mjini vyote, navyo ni nyara zake zote, uvitwae viwe mateka kwako; nawe utakula nyara za adui zako alizokupa BWANA, Mungu wako.
Basi Yoshua akaipiga nchi hiyo yote, nchi ya vilima, na nchi ya Negebu, na nchi ya Shefela, na nchi ya materemko, na wafalme wake wote; hakumwacha aliyesalia hata mmoja; lakini akawaharibu kabisa wote waliokuwa hai, kama BWANA, Mungu wa Israeli, alivyoamuru.
Tena nyara zote za miji hiyo, na wanyama wa miji, wana wa Israeli walitwaa kuwa nyara zao wenyewe; lakini kila mtu wakampiga kwa makali ya upanga, hadi walipokuwa wamewaangamiza wote, wala hawakumsaza mmoja mwenye kuvuta pumzi.
Basi wakaangamiza kabisa vitu vyote vilivyokuwa ndani ya mji, wanaume, wanawake, watoto na wazee, na ng'ombe, kondoo na punda, kwa upanga.
Wote walioanguka siku hiyo wanaume kwa wanawake, walikuwa ni elfu kumi na mbili, yaani, watu wote wa mji wa Ai.
Basi sasa nenda ukawapige Waamaleki, na kuviharibu kabisa vitu vyote walivyonavyo, wala msiwaachilie; bali waueni, mwanamume na mwanamke, na mtoto anyonyaye, ng'ombe na kondoo, ngamia na punda.