Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Hesabu 3:16 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Basi Musa akawahesabu kama alivyoagizwa na neno la BWANA.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Basi, Mose akawahesabu kufuatana na neno la Mwenyezi-Mungu, kama alivyomwamuru.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Basi, Mose akawahesabu kufuatana na neno la Mwenyezi-Mungu, kama alivyomwamuru.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Basi, Mose akawahesabu kufuatana na neno la Mwenyezi-Mungu, kama alivyomwamuru.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Kwa hiyo Musa akawahesabu, kama alivyoamriwa na neno la Mwenyezi Mungu.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Kwa hiyo Musa akawahesabu, kama alivyoamriwa na neno la bwana.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Basi Musa akawahesabu kama alivyoagizwa na neno la BWANA.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Hesabu 3:16
11 Marejeleo ya Msalaba  

Ndivyo walivyofanya wana wa Israeli. Yusufu akawapa magari kama Farao alivyoamuru, akawapa na chakula cha njiani.


Uwahesabu wana wa Lawi kwa kufuata nyumba za baba zao na jamaa zao; kila mwanamume kuanzia umri wa mwezi mmoja na zaidi utawahesabu.


Na wana wa Lawi walikuwa ni hawa kwa majina yao; Gershoni, na Kohathi, na Merari.


Hao wote waliohesabiwa katika Walawi, ambao Musa na Haruni waliwahesabu kwa amri ya BWANA, kwa jamaa zao, wanaume wote kuanzia umri wa mwezi mmoja na zaidi, walikuwa elfu ishirini na mbili.


kisha hizo fedha za ukombozi Musa akampa Haruni na wanawe, kama neno la BWANA, kama BWANA alivyomwagiza Musa.


Utumishi wote wa wana wa Wagershoni, katika mzigo wao wote, na utumishi wao wote, utakuwa kwa amri ya Haruni na wanawe; nanyi mtawaagizia mzigo wao wote kuulinda.


Hao ndio waliohesabiwa katika jamaa za Wakohathi, wote waliotumika katika hema ya kukutania, ambao Musa na Haruni waliwahesabu kwa amri ya BWANA kwa mkono wa Musa.


Hao ndio waliohesabiwa katika jamaa za wana wa Gershoni, wote waliotumika katika hema ya kukutania, ambao Musa na Haruni waliwahesabu kwa amri ya BWANA.


Hao ndio waliohesabiwa katika jamaa za wana wa Merari, ambao Musa na; Haruni waliwahesabu kwa amri ya BWANA, kwa mkono wa Musa.


Kwa amri ya BWANA, walihesabiwa kwa mkono wa Musa, kila mtu kwa utumishi wake, na kama mzigo wake ulivyokuwa; ndivyo walivyohesabiwa na yeye, kama BWANA alivyomwagiza Musa.


nao makuhani wana wa Lawi wasongee karibu, kwa kuwa ndio aliowachagua BWANA, Mungu wako, wamtumikie, na kubariki katika jina la BWANA na kila neno lishindaniwalo, na kila pigo, litakuwa kwa kufuata maneno yao;