Hesabu 26:63 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Hao ndio waliohesabiwa na Musa na Eleazari kuhani; ambao waliwahesabu wana wa Israeli katika nchi tambarare za Moabu, karibu na Yordani, hapo Yeriko. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hao ndio wanaume Waisraeli walioorodheshwa na Mose na kuhani Eleazari katika nchi tambarare za Moabu, ngambo ya mto Yordani, karibu na Yeriko. Biblia Habari Njema - BHND Hao ndio wanaume Waisraeli walioorodheshwa na Mose na kuhani Eleazari katika nchi tambarare za Moabu, ngambo ya mto Yordani, karibu na Yeriko. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hao ndio wanaume Waisraeli walioorodheshwa na Mose na kuhani Eleazari katika nchi tambarare za Moabu, ng'ambo ya mto Yordani, karibu na Yeriko. Neno: Bibilia Takatifu Hawa ndio walioorodheshwa na Musa na kuhani Eleazari wakati waliwahesabu Waisraeli kwenye nchi tambarare ya Moabu, kando ya Yordani, ng’ambo ya Yeriko. Neno: Maandiko Matakatifu Hawa ndio walioorodheshwa na Musa na kuhani Eleazari wakati waliwahesabu Waisraeli kwenye nchi tambarare ya Moabu, kando ya Yordani ng’ambo ya Yeriko. BIBLIA KISWAHILI Hao ndio waliohesabiwa na Musa na Eleazari kuhani; ambao waliwahesabu wana wa Israeli katika nchi tambarare za Moabu, karibu na Yordani, hapo Yeriko. |
Kisha Musa na Eleazari kuhani wakanena nao katika nchi tambarare za Moabu karibu na mto wa Yordani, huko Yeriko, wakawaambia,
Na hao waliohesabiwa kwao walikuwa elfu ishirini na tatu, kila mwanamume tangu huyo aliyepata umri wa mwezi mmoja, na zaidi; kwa kuwa hawakuhesabiwa katika wana wa Israeli, kwa sababu hawakupewa urithi katika wana wa Israeli.
Lakini katika watu hao hapakuwa na mtu hata mmoja wa wale waliohesabiwa na Musa na Haruni kuhani; waliowahesabu wana wa Israeli katika bara ya Sinai.
Kwa kuwa wana wa Israeli walitembea muda wa miaka arubaini barani, hadi hilo taifa zima, yaani, watu wanaume wapiganaji vita, waliotoka Misri, walipokuwa wameangamia; kwa sababu hawakuisikiza sauti ya BWANA; nao ndio BWANA aliowaapia ya kwamba hatawaacha waione hiyo nchi, ambayo BWANA aliwaapia baba zao kwamba atatupa sisi; nchi itiririkayo maziwa na asali.