Israeli akanyosha mkono wake wa kulia akauweka juu ya kichwa cha Efraimu, aliyekuwa mdogo, na mkono wake wa kushoto akauweka juu ya kichwa cha Manase, huku akijua atiavyo mikono; maana Manase ndiye aliyezaliwa kwanza.
Hesabu 26:29 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Wana wa Manase; wa Makiri, jamaa ya Wamakiri; na Makiri akamzaa Gileadi; wa Gileadi, jamaa ya Wagileadi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kabila la Manase lilikuwa na jamaa ya: Makiri, Gileadi. Biblia Habari Njema - BHND Kabila la Manase lilikuwa na jamaa ya: Makiri, Gileadi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kabila la Manase lilikuwa na jamaa ya: Makiri, Gileadi. Neno: Bibilia Takatifu Wazao wa Manase: kutoka kwa Makiri, ukoo wa Wamakiri (Makiri alikuwa baba wa Gileadi); kutoka kwa Gileadi, ukoo wa Wagileadi. Neno: Maandiko Matakatifu Wazao wa Manase: kutoka kwa Makiri, ukoo wa Wamakiri (Makiri alikuwa baba wa Gileadi); kutoka kwa Gileadi, ukoo wa Wagileadi. BIBLIA KISWAHILI Wana wa Manase; wa Makiri, jamaa ya Wamakiri; na Makiri akamzaa Gileadi; wa Gileadi, jamaa ya Wagileadi. |
Israeli akanyosha mkono wake wa kulia akauweka juu ya kichwa cha Efraimu, aliyekuwa mdogo, na mkono wake wa kushoto akauweka juu ya kichwa cha Manase, huku akijua atiavyo mikono; maana Manase ndiye aliyezaliwa kwanza.
Yusufu akaona wana wa Efraimu hata kizazi cha tatu; na wana wa Makiri, mwana wa Manase, walizaliwa magotini mwa Yusufu.
Na baadaye Hesroni akamwingilia binti wa Makiri, babaye Gileadi; ambaye alimtwaa alipokuwa na umri wa miaka sitini; naye akamzalia Segubu.
Kisha wale wakuu wa nyumba za mababa ya jamaa ya wana wa Gileadi, mwana wa Makiri, mwana wa Manase, katika jamaa za wana wa Yusufu, wakakaribia, na kunena mbele ya Musa, na mbele ya wakuu walio juu ya nyumba za mababa ya wana wa Israeli;
Hii ndiyo sehemu waliyopewa kabila la Manase; maana, yeye alikuwa ni mzaliwa wa kwanza, wa Yusufu. Na Makiri, mzaliwa wa kwanza wa Manase, babaye Gileadi, kwa sababu alikuwa mtu wa vita, basi alikuwa na Gileadi na Bashani.
Kutoka Efraimu waliteremka wao ambao shina lao ni katika Amaleki, Nyuma yako, Benyamini, kati ya watu wako. Kutoka Makiri walishuka makamanda, Na kutoka Zabuloni wao washikao fimbo ya mwandishi.