Na Timna alikuwa suria wa Elifazi, mwana wa Esau; naye akamzalia Elifazi Amaleki. Hao ndio wana wa Ada, mkewe Esau.
Hesabu 24:20 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kisha akamwangalia Amaleki, akatunga mithali yake, akasema, Amaleki alikuwa ni wa kwanza wa mataifa; Lakini mwisho wake atapata uharibifu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kisha Balaamu akawaangalia Waamaleki, akatoa kauli hii: “Amaleki ni taifa lenye nguvu kuliko yote, lakini mwishoni litaangamia kabisa.” Biblia Habari Njema - BHND Kisha Balaamu akawaangalia Waamaleki, akatoa kauli hii: “Amaleki ni taifa lenye nguvu kuliko yote, lakini mwishoni litaangamia kabisa.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kisha Balaamu akawaangalia Waamaleki, akatoa kauli hii: “Amaleki ni taifa lenye nguvu kuliko yote, lakini mwishoni litaangamia kabisa.” Neno: Bibilia Takatifu Kisha Balaamu akawaona watu wa Amaleki, na kutoa ujumbe wake: “Amaleki alikuwa ya kwanza miongoni mwa mataifa, lakini mwisho wake ataangamizwa milele.” Neno: Maandiko Matakatifu Kisha Balaamu akawaona watu wa Amaleki, na kutoa ujumbe wake: “Amaleki ilikuwa ya kwanza miongoni mwa mataifa, lakini mwisho wake itaangamizwa milele.” BIBLIA KISWAHILI Kisha akamwangalia Amaleki, akatunga mithali yake, akasema, Amaleki alikuwa ni wa kwanza wa mataifa; Lakini mwisho wake atapata uharibifu. |
Na Timna alikuwa suria wa Elifazi, mwana wa Esau; naye akamzalia Elifazi Amaleki. Hao ndio wana wa Ada, mkewe Esau.
Baada ya hayo mfalme Ahasuero alimpandisha cheo Hamani mwana wa Hamedatha, Mwagagi, akamwinua, akamwekea kiti chake juu ya wakuu wote waliokuwapo pamoja naye.
Mfalme akaamuru ifanyike vivyo hivyo, mbiu ikapigwa huko Susa, wakawatundika wale wana kumi wa Hamani.
BWANA akamwambia Musa, Andika habari hii katika kitabu iwe ukumbusho, kisha ihubiri masikioni mwa Yoshua; ya kuwa nitaufuta ukumbusho wa Amaleki kabisa, usiwe tena chini ya mbingu.
Lakini merikebu zitakuja kutoka pwani kwa Kitimu, Nazo zitamtaabisha Ashuru, na Eberi zitamtaabisha, Yeye naye atapata uharibifu.
Maji yatatiririka kutoka ndoo zake, Na mbegu zake zitakuwa katika maji mengi. Na mfalme wake ataadhimishwa kuliko Agagi, Na ufalme wake utatukuzwa.
Basi ikawa, hapo Israeli walipokuwa wamepanda mashamba, Wamidiani wakakwea, na Waamaleki, na hao wana wa mashariki; wakawavamia;
Naye kwa ushujaa, akawapiga Waamaleki, na kuwaokoa Waisraeli kutoka kwa mikono ya waliowateka nyara.
BWANA wa majeshi asema hivi, Nimeyatia moyoni mwangu yale ambayo Waamaleki waliwatenda Waisraeli, jinsi walivyowapinga njiani, hapo walipopanda kutoka Misri.
Ikawa, Daudi na watu wake walipokuwa wamefika Siklagi siku ya tatu, hao Waamaleki walikuwa wameshambulia Negebu, na Siklagi, nao wameupiga Siklagi, na kuuchoma moto;
Naye Daudi akawapiga tangu ukungu wa jioni hadi jioni ya siku ya pili; hakuna aliyeokoka, ila vijana mia nne waliopanda ngamia na kukimbia.