Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Hesabu 23:24 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Tazama, watu hawa wanaondoka kama simba jike, Na kama simba anajiinua nafsi yake, Hatalala hadi atakapokula mawindo, Na kunywa damu yao waliouawa.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Tazama! Waisraeli wameinuka kama simba jike, wanasimama kama simba dume. Ni kama simba asiyelala mpaka amalize mawindo yake, na kunywa damu ya mawindo.”

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Tazama! Waisraeli wameinuka kama simba jike, wanasimama kama simba dume. Ni kama simba asiyelala mpaka amalize mawindo yake, na kunywa damu ya mawindo.”

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Tazama! Waisraeli wameinuka kama simba jike, wanasimama kama simba dume. Ni kama simba asiyelala mpaka amalize mawindo yake, na kunywa damu ya mawindo.”

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Taifa lainuka kama simba jike; linajiinua kama simba ambaye hatulii hadi amalize kurarua mawindo yake na kunywa damu ya mawindo yake.”

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Taifa lainuka kama simba jike; linajiinua kama simba ambaye hatulii mpaka amalize kurarua mawindo yake na kunywa damu ya mawindo yake.”

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Tazama, watu hawa wanaondoka kama simba jike, Na kama simba anajiinua nafsi yake, Hatalala hadi atakapokula mawindo, Na kunywa damu yao waliouawa.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Hesabu 23:24
20 Marejeleo ya Msalaba  

Benyamini ni mbwamwitu mwenye kuraruararua Asubuhi atakula mawindo, Na jioni atagawanya mateka.


Yuda ni mwanasimba, Kutoka katika mawindo, mwanangu, umepanda; Aliinama akajilaza kama simba, Na kama simba mke; ni nani atakayemwamsha?


Na simba kumi na wawili wamesimama juu ya ngazi sita huku na huko; wala hakikufanyika kwa mkono wake katika ufalme wowote.


Kiti kile kilikuwa na ngazi sita, tena na kikao cha miguu cha dhahabu, navyo vilikuwa vimeshikamana na kiti; na kila upande wa kiti hicho palikuwa na pakuengemeza mikono, na simba wawili walisimama kando ya hiyo mikono.


Kama mfano wa simba atakaye kurarua, Kama mwanasimba aoteaye katika maotea yake.


Simba aliye hodari kupita wanyama wote; Wala hatishwi na mwingine yeyote yule;


Maana BWANA aniambia hivi, Kama vile ilivyo simba angurumapo na mwanasimba juu ya mawindo yake, wachungaji wengi wakiitwa ili kumpiga, lakini hatiwi hofu na sauti zao, wala kufanya woga kwa sababu ya mshindo wao; ndivyo BWANA wa majeshi atakavyoshuka ili kufanya vita juu ya mlima Sayuni, na juu ya kilima chake.


Na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake; bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele.


Simba amekwisha kunguruma, ni nani asiyeogopa? Bwana MUNGU amenena, ni nani awezaye neno ila kutabiri?


Kao la simba li wapi? Na mahali walishapo wanasimba pa wapi, mahali walipotembea simba mume na simba mke na mwanasimba, wala hapana aliyewatia hofu?


Simba alirarua vipande vipande chakula cha kuwatosha watoto wake, aliwakamatia majike wake mawindo, aliyajaza mapango yake mateka, na makao yake aliyajaza nyama iliyoraruliwa.


Siku hiyo nitawafanya wakuu wa Yuda kuwa kama kigae chenye moto katika kuni, na kama kinga cha moto katika miganda; nao watateketeza watu wa kila kabila, wawazungukao pande zote, upande wa mkono wa kulia na upande wa mkono wa kushoto; na baada ya haya Yerusalemu utakaa mahali pake, naam, hapo Yerusalemu.


Balaki akamwambia Balaamu, Basi usiwalaani kabisa, wala usiwabariki kabisa.


Namwona, lakini si sasa; Namtazama, lakini si karibu; Nyota itatokea katika Yakobo Na fimbo ya enzi itainuka katika Israeli; Nayo itazipigapiga pembe za Moabu, Na kuwavunjavunja wana wote wa ghasia.


Na Gadi akamnena, Na abarikiwe amwongezaye Gadi; Yeye hukaa kama simba mke, Hurarua mkono, naam, na utosi wa kichwa.


Na mmojawapo wa wale wazee akaniambia, Usilie; tazama, Simba aliye wa kabila la Yuda, Shina la Daudi, yeye ameshinda apate kukifungua kile kitabu, na ile mihuri yake saba.