nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka;
Hesabu 23:20 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Tazama, nimepewa amri kubariki, Yeye amebariki, nami siwezi kulitangua. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Tazama, nimepewa amri ya kubariki, naye amebariki wala siwezi kuitangua. Biblia Habari Njema - BHND Tazama, nimepewa amri ya kubariki, naye amebariki wala siwezi kuitangua. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Tazama, nimepewa amri ya kubariki, naye amebariki wala siwezi kuitangua. Neno: Bibilia Takatifu Nimepokea agizo kubariki; amebariki, nami siwezi kubadilisha. Neno: Maandiko Matakatifu Nimepokea agizo kubariki; amebariki, nami siwezi kubadilisha. BIBLIA KISWAHILI Tazama, nimepewa amri kubariki, Yeye amebariki, nami siwezi kulitangua. |
nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka;
katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki lango la adui zao;
Isaka akatetemeka tetemeko kuu sana, akasema, Ni nani basi yule aliyetwaa mawindo akaniletea? Nami nimekwisha kula kabla hujaja wewe, nikambariki; naam, naye atabarikiwa.
nawe sasa umekuwa radhi kuibarikia nyumba ya mtumishi wako, ipate kudumu milele mbele zako; kwa maana wewe, BWANA, umebarikia, nayo imebarikiwa milele.
Naam, tangu siku ya leo, mimi ndiye; wala hakuna awezaye kuokoa katika mkono wangu; mimi nitatenda kazi, naye ni nani awezaye kuizuia?
Mungu akamwambia Balaamu, Usiende pamoja nao; wala usiwalaani watu hawa, maana wamebarikiwa.
Balaamu akajibu akawaambia watumishi wa Balaki, Hata kama Balaki angenipa nyumba yake imejaa fedha na dhahabu, siwezi kukiuka neno la BWANA, Mungu wangu, kulipunguza au kuliongeza.
Balaamu akamwambia Balaki, Tazama, nimekujia. Je! Mimi sasa nina uwezo wowote kusema neno lolote? Neno lile Mungu atakalolitia kinywani mwangu, ndilo nitakalolisema.
Nanyi mnalindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya imani ili mpate wokovu ulio tayari kufunuliwa wakati wa mwisho.