Mungu akapaita pale pakavu Nchi; na makusanyiko ya maji akayaita Bahari; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
Hesabu 20:29 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na mkutano wote ulipoona ya kuwa Haruni amekufa, wakamwombolezea Haruni muda wa siku thelathini, maana, nyumba yote ya Israeli ikamwombolezea. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Jumuiya yote ya watu ilipopata habari kwamba Aroni amefariki, ikafanya matanga ya siku thelathini. Biblia Habari Njema - BHND Jumuiya yote ya watu ilipopata habari kwamba Aroni amefariki, ikafanya matanga ya siku thelathini. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Jumuiya yote ya watu ilipopata habari kwamba Aroni amefariki, ikafanya matanga ya siku thelathini. Neno: Bibilia Takatifu Jumuiya yote walipofahamu kwamba Haruni amekufa, Waisraeli wote wakamwomboleza kwa siku thelathini. Neno: Maandiko Matakatifu Jumuiya yote ilipofahamu kwamba Haruni amekufa, jamaa yote ya Kiisraeli wakamwomboleza kwa siku thelathini. BIBLIA KISWAHILI Na mkutano wote ulipoona ya kuwa Haruni amekufa, wakamwombolezea Haruni muda wa siku thelathini, maana, nyumba yote ya Israeli ikamwombolezea. |
Mungu akapaita pale pakavu Nchi; na makusanyiko ya maji akayaita Bahari; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
Mungu akaiita nuru Mchana, na giza akaliita Usiku. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya kwanza.
Sara akafa katika Kiriath-arba, ndio Hebroni, katika nchi ya Kanaani. Abrahamu akamlilia na kumwombolezea Sara.
Wakaja mpaka uwanja wa kupuria nafaka wa Atadi, uliyo ng'ambo ya Yordani. Wakaomboleza huko maombolezo makuu, mazito sana. Akafanya matanga ya baba yake siku saba.
Siku zake arubaini zikaisha, maana siku hizo zilitimiza siku za wale waliohifadhiwa kwa kupakwa dawa. Wamisri wakamwombolezea siku sabini.
Wana wa Israeli wakamwombolezea Musa katika uwanda wa Moabu siku thelathini; basi siku za maombolezo ya matanga ya Musa zikaisha.
Akafa Samweli; nao Israeli wote wakakusanyika, wakamwomboleza, wakamzika nyumbani mwake huko Rama. Kisha Daudi akaondoka, akashuka mpaka nyikani mwa Maoni.