Hesabu 16:35 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kisha moto ukatoka kwa BWANA, ukawateketeza hao watu mia mbili hamsini waliofukiza uvumba. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kisha Mwenyezi-Mungu akapeleka moto ukawateketeza wale watu 250 waliokwenda kufukiza ubani. Biblia Habari Njema - BHND Kisha Mwenyezi-Mungu akapeleka moto ukawateketeza wale watu 250 waliokwenda kufukiza ubani. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kisha Mwenyezi-Mungu akapeleka moto ukawateketeza wale watu 250 waliokwenda kufukiza ubani. Neno: Bibilia Takatifu Moto ukaja kutoka kwa Mwenyezi Mungu, ukawateketeza wale watu mia mbili na hamsini waliokuwa wakifukiza uvumba. Neno: Maandiko Matakatifu Moto ukaja kutoka kwa bwana, ukawateketeza wale watu 250 waliokuwa wakifukiza uvumba. BIBLIA KISWAHILI Kisha moto ukatoka kwa BWANA, ukawateketeza hao watu mia mbili hamsini waliofukiza uvumba. |
Mungu wetu atakuja wala sio kimya kimya, Moto utakula mbele zake, na tufani yavuma sana ikimzunguka pande zote.
Na watu sabini wa wazee wa Israeli walikuwa wamesimama na kuzielekea, na katikati yao alisimama Yaazania, mwana wa Shafani; kila mmoja ana chetezo mkononi mwake, na harufu ya moshi wa uvumba ilipaa juu.
mkatwae kila mtu chetezo chake, na kutia uvumba juu yake, mkavilete mbele za BWANA, vyetezo mia mbili na hamsini; wewe pia, na Haruni, kila mtu na awe na chetezo chake.
nao, pamoja na watu kadhaa wa wana wa Israeli, watu mia mbili na hamsini, Wakuu wa mkutano, waliokuwa wateule wa mkutano, watu wenye sifa, wakainuka mbele ya Musa;
Nao Israeli wote waliokuwa kandokando yao wakakimbia kwa ajili ya kilio chao; kwa kuwa walisema, Nchi isije kutumeza na sisi.
Basi waliokufa kwa tauni walikuwa elfu kumi na nne na mia saba, zaidi ya hao waliokufa katika jambo la Kora.
nchi ikafunua kinywa chake, na kuwameza pamoja na Kora, mkutano huo ulipokufa; wakati moto ulipowateketeza watu mia mbili na hamsini, nao wakawa ishara.
Kisha Nadabu na Abihu walikufa mbele za BWANA, waliposongeza moto wa kigeni mbele za BWANA, katika jangwa la Sinai, nao walikuwa hawana wana; na Eleazari na Ithamari wakafanya kazi ya ukuhani wakati wa uhai wa Haruni baba yao.
Na mtu akitaka kuwadhuru, moto hutoka katika vinywa vyao na kuwala adui zao. Na mtu akitaka kuwadhuru, hivyo ndivyo impasavyo kuuawa.