Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Hesabu 16:29 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Kama watu hawa wakifa kifo cha kawaida, kama watu wote wafavyo, au kama wataadhibiwa kwa adhabu ya watu wote; hapo basi BWANA hakunituma mimi.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Watu hawa wakifa kifo cha kawaida, au wakipatwa na maafa kama watu wengine, basi jueni kuwa Mwenyezi-Mungu hakunituma.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Watu hawa wakifa kifo cha kawaida, au wakipatwa na maafa kama watu wengine, basi jueni kuwa Mwenyezi-Mungu hakunituma.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Watu hawa wakifa kifo cha kawaida, au wakipatwa na maafa kama watu wengine, basi jueni kuwa Mwenyezi-Mungu hakunituma.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Ikiwa watu hawa watakufa kifo cha kawaida na kupatwa na yale ya kawaida yanayowapata wanadamu, basi Mwenyezi Mungu hakunituma mimi.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Ikiwa watu hawa watakufa kifo cha kawaida na kupatwa na yale ya kawaida yanayowapata wanadamu, basi bwana hakunituma mimi.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Kama watu hawa wakifa kifo cha kawaida, kama watu wote wafavyo, au kama wataadhibiwa kwa adhabu ya watu wote; hapo basi BWANA hakunituma mimi.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Hesabu 16:29
11 Marejeleo ya Msalaba  

Ikawa, wakati wa kutoa dhabihu ya jioni, Eliya nabii akakaribia, akasema, Ee BWANA, Mungu wa Abrahamu, na wa Isaka, na wa Israeli, na ijulikane leo ya kuwa wewe ndiwe Mungu katika Israeli, na ya kuwa mimi ni mtumishi wako, na ya kuwa nimefanya mambo haya yote kwa neno lako.


Mikaya akasema, Ukirudi kabisa kwa amani, BWANA hakusema kwa mimi. Akasema, Sikieni, enyi watu wote.


Mikaya akasema, Ukirudi kabisa kwa amani, BWANA hakusema kupitia kwangu. Akasema, Sikieni, enyi watu wote.


Lakini sasa, kwa sababu yeye hakukujia katika hasira zake, Wala hauzingatii sana makosa;


Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,


Basi sasa uende ukawaongoze watu hawa mpaka mahali pale ambapo nimekwambia habari zake; tazama, malaika wangu atakutangulia; pamoja na hayo siku nitakayowajia nitawapatiliza kwa ajili ya dhambi yao.


Kwa maana linalowatukia wanadamu linawatukia wanyama; jambo moja lawatukia; anavyokufa huyu ndivyo anavyokufa huyu; naam, wote wanayo pumzi moja; wala mwanadamu hana kitu cha kumpita mnyama; kwa maana yote ni ubatili.


Nanyi mtafanya nini siku ya kujiliwa, na wakati wa uangamivu, utakaokuja kutoka mbali sana? Je! Mtamkimbilia nani mpate msaada? Na utukufu wenu mtauacha wapi?


Je! Nisiwapatilize kwa sababu ya mambo hayo? Asema BWANA; na nafsi yangu, je! Nisijilipizie kisasi juu ya taifa la namna hii?


Adhabu ya uovu wako imetimia, Ee binti Sayuni; Hatakuhamisha tena; Atapatiliza uovu wako, Ee binti Edomu; Atazivumbua dhambi zako.


Na mtu akitaka kuwadhuru, moto hutoka katika vinywa vyao na kuwala adui zao. Na mtu akitaka kuwadhuru, hivyo ndivyo impasavyo kuuawa.