naye akatoka ili amlaki Asa, akamwambia, Nisikieni, Ee Asa, na Yuda wote na Benyamini; BWANA yu pamoja nanyi, mkiwa pamoja naye; nanyi mkimtafuta ataonekana kwenu; lakini mkimwacha atawaacha ninyi.
Hesabu 14:42 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Msikwee, kwa kuwa BWANA hayumo kati yenu; msipigwe na kuangushwa mbele ya adui zenu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Msiende huko milimani msije mkapigwa bure na adui zenu, maana, Mwenyezi-Mungu hayuko pamoja nanyi. Biblia Habari Njema - BHND Msiende huko milimani msije mkapigwa bure na adui zenu, maana, Mwenyezi-Mungu hayuko pamoja nanyi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Msiende huko milimani msije mkapigwa bure na adui zenu, maana, Mwenyezi-Mungu hayuko pamoja nanyi. Neno: Bibilia Takatifu Msipande juu, kwa kuwa Mwenyezi Mungu hayupo pamoja nanyi. Mtashindwa na adui zenu, Neno: Maandiko Matakatifu Msipande juu, kwa kuwa bwana hayupo pamoja nanyi. Mtashindwa na adui zenu, BIBLIA KISWAHILI Msikwee, kwa kuwa BWANA hayumo kati yenu; msipigwe na kuangushwa mbele ya adui zenu. |
naye akatoka ili amlaki Asa, akamwambia, Nisikieni, Ee Asa, na Yuda wote na Benyamini; BWANA yu pamoja nanyi, mkiwa pamoja naye; nanyi mkimtafuta ataonekana kwenu; lakini mkimwacha atawaacha ninyi.
Kwa kuwa Mwamaleki na Mkanaani wako mbele yenu, nanyi mtaanguka kwa upanga, kwa sababu mmerudi nyuma msimfuate BWANA, kwa hiyo BWANA hatakuwa pamoja nanyi.
BWANA akaniambia, Waambie, Msiende, wala msipigane; kwani mimi siko kati yenu; msije mkapigwa mbele ya adui zenu.
Ndipo hasira yangu itakapowaka juu yao siku hiyo, nami nitawaacha, nitawaficha uso wangu, nao wataliwa, tena watajiliwa na mambo maovu mengi na mashaka; hata waseme siku hiyo, Je! Kujiliwa kwetu na maovu haya si kwa sababu Mungu wetu hayumo kati yetu?
Ndiposa wana wa Israeli hawawezi kusimama mbele ya adui zao; wakawapa visogo adui zao, kwa sababu wamelaaniwa; mimi sitakuwa pamoja nanyi tena, msipokiharibu kitu kile mlicho nacho kilichowekwa wakfu.
Kisha akasema, Samsoni, Wafilisti wanakujia. Akaamka katika usingizi wake, akasema, Nitakwenda nje kama siku nyingine, na kujinyosha. Lakini hakujua ya kuwa BWANA amemwacha.