Hesabu 14:39 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kisha Musa akawaambia wana wa Israeli wote maneno haya, na hao watu wakaomboleza sana. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Naye Mose aliwaambia Waisraeli wote nao walilia kwa uchungu mwingi. Biblia Habari Njema - BHND Naye Mose aliwaambia Waisraeli wote nao walilia kwa uchungu mwingi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Naye Mose aliwaambia Waisraeli wote nao walilia kwa uchungu mwingi. Neno: Bibilia Takatifu Musa alipotoa taarifa hii kwa Waisraeli wote, waliomboleza kwa uchungu. Neno: Maandiko Matakatifu Musa alipotoa taarifa hii kwa Waisraeli wote, waliomboleza kwa uchungu. BIBLIA KISWAHILI Kisha Musa akawaambia wana wa Israeli wote maneno haya, na hao watu wakaomboleza sana. |
BWANA, katika taabu zao walikwenda kwako; waliomba maombi mengi wakati adhabu yako ilipokuwa juu yao.
Waambieni, Kama niishivyo, asema BWANA, hakika yangu kama ninyi mlivyonena masikioni mwangu, ndivyo nitakavyowafanyia ninyi;
Lakini Yoshua mwana wa Nuni, na Kalebu mwana wa Yefune, wakabaki hai miongoni mwa wale watu waliokwenda kuipeleleza nchi.
bali wana wa ufalme watatupwa katika giza la nje, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.
Maana mnajua ya kuwa hata alipotaka baadaye kuirithi baraka, alikataliwa (maana hakuona nafasi ya kutubu), ijapokuwa aliitafuta sana kwa machozi.
Ndiposa wana wa Israeli hawawezi kusimama mbele ya adui zao; wakawapa visogo adui zao, kwa sababu wamelaaniwa; mimi sitakuwa pamoja nanyi tena, msipokiharibu kitu kile mlicho nacho kilichowekwa wakfu.