Hesabu 14:29 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC mizoga yenu itaanguka katika jangwa hili, na wote waliohesabiwa miongoni mwenu, kama jumla ya hesabu yenu, tangu waliopata umri wa miaka ishirini na zaidi, hao walioninung'unikia, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mtakufa na miili yenu itatupwa humuhumu jangwani, kwa sababu mmenungunika dhidi yangu, hakuna hata mmoja wenu mwenye umri wa kuanzia miaka ishirini na zaidi, Biblia Habari Njema - BHND Mtakufa na miili yenu itatupwa humuhumu jangwani, kwa sababu mmenungunika dhidi yangu, hakuna hata mmoja wenu mwenye umri wa kuanzia miaka ishirini na zaidi, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mtakufa na miili yenu itatupwa humuhumu jangwani, kwa sababu mmenung'unika dhidi yangu, hakuna hata mmoja wenu mwenye umri wa kuanzia miaka ishirini na zaidi, Neno: Bibilia Takatifu Kila mmoja wenu mwenye umri wa miaka ishirini au zaidi ambaye alihesabiwa na amenung’unika dhidi yangu, miili yenu itaanguka katika jangwa hili. Neno: Maandiko Matakatifu Kila mmoja wenu mwenye umri wa miaka ishirini au zaidi ambaye alihesabiwa na amenung’unika dhidi yangu, miili yenu itaanguka katika jangwa hili. BIBLIA KISWAHILI mizoga yenu itaanguka katika jangwa hili, na wote waliohesabiwa miongoni mwenu, kama jumla ya hesabu yenu, tangu waliopata umri wa miaka ishirini na zaidi, hao walioninung'unikia, |
Nami nitawasafisha kwa kuwatoa waasi, na hao walionikosa; nitawatoa katika nchi wanayokaa ugenini, lakini hawataingia katika nchi ya Israeli; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.
Basi hao wote waliohesabiwa katika wana wa Israeli kwa kufuata nyumba za baba zao kuanzia umri wa miaka ishirini na zaidi; wote walioweza kwenda vitani katika Israeli;
hao wote waliohesabiwa walikuwa ni wanaume elfu mia sita na tatu, mia tano na hamsini (603,550).
Lakini katika watu hao hapakuwa na mtu hata mmoja wa wale waliohesabiwa na Musa na Haruni kuhani; waliowahesabu wana wa Israeli katika bara ya Sinai.
Kwa kuwa BWANA alisema juu yao, Hapana budi watakufa nyikani. Napo hapakusalia mtu mmoja miongoni mwao, isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune, na Yoshua mwana wa Nuni.
Na siku tulizokuwa tukienda kutoka Kadesh-barnea hata tulipovuka kijito cha Zeredi, ilikuwa ni miaka thelathini na minane; maana, hata walipokwisha kuangamizwa watu wa vita kutoka kati ya kambi, kizazi chao chote, kama walivyoapiwa na BWANA.
Tena ni akina nani aliochukizwa nao miaka arubaini? Si wale waliokosa, ambao mizoga yao ilianguka katika jangwa?
Kwa kuwa wana wa Israeli walitembea muda wa miaka arubaini barani, hadi hilo taifa zima, yaani, watu wanaume wapiganaji vita, waliotoka Misri, walipokuwa wameangamia; kwa sababu hawakuisikiza sauti ya BWANA; nao ndio BWANA aliowaapia ya kwamba hatawaacha waione hiyo nchi, ambayo BWANA aliwaapia baba zao kwamba atatupa sisi; nchi itiririkayo maziwa na asali.
Tena napenda kuwakumbusha, ijapokuwa mmekwisha kujua haya yote, ya kwamba Bwana, akiisha kuwaokoa watu katika nchi ya Misri, aliwaangamiza baadaye wale wasioamini.