Akasema ya kuwa atawaangamiza Kama Musa, mteule wake, asingalisimama, Mbele zake na kusimama palipobomoka, Ili aigeuze hasira yake asije akawaangamiza.
Hesabu 14:20 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC BWANA akasema, Mimi nimewasamehe kama neno lako lilivyokuwa; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenyezi-Mungu akajibu, “Nimewasamehe kama ulivyoomba. Biblia Habari Njema - BHND Mwenyezi-Mungu akajibu, “Nimewasamehe kama ulivyoomba. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenyezi-Mungu akajibu, “Nimewasamehe kama ulivyoomba. Neno: Bibilia Takatifu Mwenyezi Mungu akajibu, “Nimewasamehe kama ulivyoomba. Neno: Maandiko Matakatifu bwana akajibu, “Nimewasamehe kama ulivyoomba. BIBLIA KISWAHILI BWANA akasema, Mimi nimewasamehe kama neno lako lilivyokuwa; |
Akasema ya kuwa atawaangamiza Kama Musa, mteule wake, asingalisimama, Mbele zake na kusimama palipobomoka, Ili aigeuze hasira yake asije akawaangamiza.
Ee BWANA, Mungu wetu, ndiwe uliyewajibu; Ulikuwa kwao Mungu mwenye kusamehe Ingawa uliwapatiliza matendo yao.
Musa akamwambia Farao, Haya, ujitukuze juu yangu katika jambo hili; sema ni lini unapotaka nikuombee wewe, na watumishi wako, na watu wako, ili hao vyura waangamizwe watoke kwako wewe na nyumba zako, wakae ndani ya mto tu.
BWANA asema hivi, Watu wale walioachwa na upanga walipata neema jangwani; yaani, Israeli, hapo nilipokwenda kumstarehesha.
Basi ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, ili mpate kuponywa. Sala yake mwenye haki ina nguvu nyingi, na hutenda mengi.