Hesabu 14:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mkutano wote wakapaza sauti zao wakalia; watu wakatoka machozi usiku ule. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Jumuiya yote ya Waisraeli ikaangua kilio kikubwa, watu wakalia usiku ule. Biblia Habari Njema - BHND Jumuiya yote ya Waisraeli ikaangua kilio kikubwa, watu wakalia usiku ule. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Jumuiya yote ya Waisraeli ikaangua kilio kikubwa, watu wakalia usiku ule. Neno: Bibilia Takatifu Usiku ule watu wote wa jumuiya walipaza sauti zao na kulia kwa sauti kuu. Neno: Maandiko Matakatifu Usiku ule watu wote wa jumuiya walipaza sauti zao na kulia kwa sauti kuu. BIBLIA KISWAHILI Mkutano wote wakapaza sauti zao wakalia; watu wakatokwa machozi usiku ule. |
Ilikuwa hapo Farao alipowaacha watu hao waende zao, Mungu hakuwaongoza kwa njia ya nchi ya Wafilisti, ijapokuwa ilikuwa ni ya karibu; maana Mungu alisema, Wasije wakabadili nia watu hawa hapo watakapokumbana na vita, na kurudi Misri;
Kisha, huko tuliwaona Wanefili, wana wa Anaki, waliotoka kwa hao Wanefili; tukajiona nafsi zetu kuwa kama mapanzi; nao ndivyo walivyotuona sisi.
Kisha wana wa Israeli wote wakamnung'unikia Musa na Haruni; mkutano wote wakawaambia, Ingekuwa heri kama tungalikufa katika nchi ya Misri, au, ingekuwa heri kama tungalikufa katika jangwa hili.
Mkarudi mkalia mbele za BWANA; BWANA asiisikize sauti yenu, wala hakuelekeza masikio yake kwenu.
Na wakati alipowatuma BWANA kutoka Kadesh-barnea, akiwaambia, Kweeni mkaimiliki nchi niliyowapa; ndipo mkaasi juu ya maagizo ya BWANA, Mungu wenu, hamkumsadiki wala hamkusikiza sauti yake.
Lakini wale ndugu zangu waliokwea kwenda pamoja nami waliwavunja watu moyo; ila mimi nilimfuata BWANA, Mungu wangu, kwa utimilifu.
Ndipo Daudi na watu waliokuwa pamoja naye wakapaza sauti zao na kulia, hadi walipokuwa hawana nguvu za kulia tena.